Waziri
Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akizungumza leo na Madaktari kufuatia sakata la
mgomo wao uliodumu kwa kipindi cha zaidi ya wiki mbili sasa wakati
alipofika kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam kwa
lengo la kukutana nao na kusikiliza malalamiko yao.Pia kutokana
Malalamiko ya Madaktari hao ya kutokuwa na imani na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya,Blandina Nyoni pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali,Dkt. Deo
Mtasiwa.Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda amesema amewafuta kazi wakuu hao
kuanzia leo hii kutokana na kuonekana kuwa wao ndio kiini cha mgogoro
huo ambao umekuwa ukisababisha matatizo makubwa kwa taifa.Waziri Mkuu
amewataka Madaktari waunde kamati maalumu ambayo itakusanya mapendekezo
ya madaktari wote na kumpelekea yeye ili aweze kuyafanyia kazi,huku
akiwataka Madaktari hao kurudi kazini na kuendelea na majukumu yao kama
ilivyokuwa hapo awali.
Mh. Waziri Mkuu akisikiliza kwa makini malalamiko na mapendekezo yaliyokuwa yakitolewa na madaktari .
Baadhi ya Madaktari wa Muhimbili wakizungumza huku umati wa madaktari wengine ukiwa umetulia kusikiliza.
Madaktari wakishangilia wakati wenzao wakitoka mapendekezo mbali mbali kwa Waziri Mkuu.
Sehemu
ya Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakimsikiliza Waziri
Mkuu,Mh. Mizengo Pinda wakati akizungumza nao leo kwenye ukumbi wa
Mikutano wa Hospitali hiyo leo.
Waziri Mkuu akiagana na baadhi ya Madaktari wa Muhimbili waliokuwa nje ya ukumbi wakati akiondoka.
No comments:
Post a Comment