Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akizungumza na vyombo vya habari
mapema leo asubuhi wakati wa hafla fupi ya kutangaza majina ya
wanamuziki watakaowania tuzo za kilimanjaro Tanzania Music Award 2012
iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Meneja
Masoko wa TBL,Mamongae Mahlare akizungumza na vyombo vya habari mapema
leo asubuhi wakati wa hafla fupi ya kutangaza majina ya wanamuziki
watakaowania tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Award 2012 iliyofanyika
leo jijini Dar es Salaam.
Mratibu
wa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards ambaye pia ni mwakilishi
wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Angelo Luhala (katikati) akionyesha
karatasi yenye majina ya washiriki wanaowania tuzo hizo leo jijini Dar
es Salaam.Kulia ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe na Kulia
ni Afisa kutoka Kampuni ya Innovex ambao ndio wanaoandaa majina hayo ya
wasanii.Yafuatayo hapo chini ni majina ya washiriki na Categories zao
Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager kwa
kushirikiana na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) leo wametangaza rasmi
wateule wa vinyang’anyiro 22 vya Tuzo za Muziki Tanzania (Kilimanjaro
Tanzania Music Awards).
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, Meneja wa bia ya
Kilimanjaro Bwana George Kavishe alisema “Academy ilikaa mwisho wa wiki
iliopita na kufanya kazi ngumu na nzuri ya kuteua wasanii wa muziki
waliofanya kazi nzuri na zilizopendwa na kukubalika zaidi na wengi kwa
mwaka 2011”.
Mchakato
wa Academy ulisimamiwa na wasimamizi wa mahesabu na utawala INNOVEX ili
kuhakikisha zoezi linafanywa kwa uhuru na haki muda wote. George
Kavishe aliongeza “Kama tulivoahidi mwaka juzi na mwaka jana kwamba tuzo
zitaendeshwa kisasa na kitaalum ili kuzipatia haki na kutengeneza
mazingira ya uwazi kwa wapenzi wa muziki nchini.
Tunaendeleza
ahadi hii na ndio maana INNOVEX wameendelea kusimamia zoezi hili la
Academy pamoja na kura zote kwa mwaka huu tena.” Kura za wana Academy ni
siri na majibu ya wateule watano kwa kila kinyang’anyiro hubaki siri ya
INNOVEX hadi kutangazwa, halikadhalika na majibu ya kura za wananchi za
washindi.
Baraza
la Sanaa Tanzania kupitia kwa mwakilishi wake Nd. Angelo Luhala ambaye
ni mratibu wa Tuzo za Muziki Tanzania, nalo limeipongeza Academy kwa
kazi nzuri kwa mara ingine na kuwasii wasanii kuyapokea matokeo na
kushirikiana na waandaji katika hatua zilizobakia ili kufanikisha tuzo
hizi.
Hatua zifwatazo:
1.
Semina ya Wasanii:Wasanii wateule wa tuzo mbalimbali watapata semina
elekezi kuhusu tuzo hizi na kupata nafasi kuuliza maswali juu ya
mchakato mzima wa kupata wateule na taratibu zitakazofwata.
2.
Kura.Kura zitapigwa kwa muda wa wiki 7 kuanzia tarehe 13/ Feb - 06/ Apr
Maelekezo ya upigaji kura yatapatikana katika tovuti ya Kilimanjaro
www.kilitimetz.com na mitandao mingine pamoja na kwenye matangazo ya
magazeti na vipindi mbali mbali ya redio na TV.
3.
Usiku wa utoaji Tuzo.Kilimanjaro Tanzania Music Awards zatarajia
kufanyika tarehe 14. Aprili. 2012 katika ukumbi wa Mlimani City. Taarifa
zaidi zitafuata kupitia mitandao, redio na TV mbali mbali.
Yafuatayo hapo chini ni majina ya washiriki na Categories zao
No comments:
Post a Comment