Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu ( LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba
akizungumza na waandishi wa habari katika maeneo ya Salender Brige,
kuelezea maadamano ya wanaharakati hao ya kuishinikiza serikali kuchukua
hatua na kutatua mgogoro wa mgomo wa Madaktari wa Hospitali ya
Muhimbili, ulioanza hivi karibuni na ambao bado unaendelea.
Ameongeza kwamba hali ya wagonjwa inaendelea kuwa mbaya zaidi kwa
sababu ya mgomo huo, Dk Hellen Kijo-Bisimba mara baada ya kumalizika kwa maandamano hayo yaliyofanyika leo.
Mkurugenzi wa TAMWA, Analilea Nkya akiwa ameshikilia bango lake wakati wa maandamano hayo jijini Dar es salaam leo.
Polisi wakiwaamuru waandamanaji watawanyike mara baada ya kufika katika eneo la Salender Brige jijini Dar es salaam leo.
Mkurugenzi
wa TAMWA,Mama Ananilea Nkya (kulia) akizungumza na baadhi ya vyombo vya
habari mbalimbali kuhusiana na maandamano yao yaliyodumu kwa muda wa
masaa mawili hivi kwa ajili ya kuishinikiza Serikali ikae meza moja na
madaktari na kuhakikisha mgomo wao unakoma mara moja na kuhakikisha
shughuli za matibabu hospitali ya Muhimbili na nyinginezo zinaendelea
kama kawaida.
Amri ikitolewa kuwataka wanaharakati kuondoka eneo hilo,kwani ilielezwa kuwa maandamano hayo yamefanyika bila kubarikiwa.
Askari wakiwa eneo la tukio mapema leo jioni.
Ujumbe kutoka kwa wanaharakati hao.
Mwanaharakati akiwa na ujumbe wake.
No comments:
Post a Comment