Mshindi wa taji la Redd’s Miss Geita 2013, Salsha
Isidore (katikati) akiwa mwenye furaha wakati wa kupiga picha ya pamoja na
warembo wenzake Sia Kimambo (kulia) aliyeshika nafasi ya pili na Mshindi wa
tatu wa shindano hilo, Nurieth Rashid. Salsha aliwashinda warembo wenzake 12
waliokuwa wakiwania taji hilo pamoja nae.
****** *******
Na Father Kidevu Blog,
Geita
MREMBO Salshia Isidore
amechaguliwa kuwa Redd’s Miss Geita 2013 baada ya kuwashinda warembo wenzake 12
katika shindano lililifanyika Jumamosi
Juni 1, kwenye ukumbi wa Desire
uliopo mjini Geita.
Wengine walioingia nafasi
ya tatu bora ni pamoja na Nurieth Rashid aliyeshika nafasi ya tatu na Stella
Magerezi alishika nafasi ya pili.
Katika shindano hilo
lililosindikizwa na burudani safi kutoka kwa msanii Baby Madaha na Bob Haisa
huku mgeni rasmi akiwa ni Mbunge wa Viti Maalum wa Geita Vicky Kamata.
Washindi hao watatu
watawakilisha mkoa wa Geita kwenye shindano la Kanda ya Ziwa ili kuwapata
washiriki watakaoenda ngazi ya taifa.
Akizungumza na washindi
pamoja na warembo wengine kwa ujumla Vicky aliitaka jamii ya watu wa Geita
kuyatambua mashindano hayo kuwa ni muhimu na yanasaidia suala la ajira.
Alisema kuwa kupitia
mashindano hayo kuna mengi ambayo yanaweza kufanyika kwa kuwa mashindano hayo
ni fursa ya kuzungumza na wananchi kuielezea masuala mbalimbali ya kimaisha.
“ Najua kwa sasa hata
katika Bunge hili la bajeti kuna mengi ambayo tumeyajadili na kuyapitisha kwa
ajili ya vijana na hasa pia kupitia sanaa na hivyo mashindano kama haya
yanahusika kabisa” alisema Vicky.
Naye mwandaji wa shindano
hilo alisema kuwa washindi hao mshindi wa kwanza amepewa laki tatu, huku wa
pili amepewa laki mbili na wa tatu laki tatu.
Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora wakiwa katika picha ya pamoja.
Wanyange walioshiriki shindano la Redd's Miss Geita 2013 wakiwa katika picha ya pamoja jukwaani.
Mbunge
wa Viti Maalum kutoka Mkoani Geita, Vicky Kamata (kulia) akitoa nasaha
zake kwa washindi na warembo wote walioshiriki shindano hilo.
Majaji wa shindano hilo kutoka kushoto, Godson Mkama, Hadija na Papaa wa Disire wakiwajibika.
Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (katikati) akiwa na Mbunge Vicky Kamata.
Mwandaaji wa Miss Geita, Lady Rose akiongea machache
No comments:
Post a Comment