MWANAMKE
mkazi wa kijiji cha Ikandamoyo, wilayani Katavi, Veronica Saleh ‘Mama
Kaela’ (50), amefanya uamuzi adimu wa kuolewa na wanaume wawili ambao
anaishi nao kijijini hapo.
Kijiji
hicho kipo umbali wa takribani kilometa 30 kutoka mjini hapa katika
Jimbo la Katavi linalowakilishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Pamoja
na ndoa hiyo iliyowezeshwa na mume mkubwa kukubali kuishi na mume
mdogo, imeelezwa kuwa mwanamke huyo ndiye ‘aliyewaoa’ wanaume hao kwa
zaidi ya miaka saba sasa, huku akiwa na amri kuu katika nyumba, kama
ilivyo katika ndoa za kawaida.
Wanaume hao ni Paulo Sabuni ‘Baba Kaela’ (60) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (45) ambaye ni mume mdogo.
Taarifa
za kuwapo kwa ndoa hiyo ya aina yake, ziliifikia Globu ya Jamii na
kufanyiwa uchunguzi kwa zaidi ya wiki tatu, na hatimaye katikati ya wiki
hii, wahusika walikubali wao wenyewe kuzungumzia suala hilo. Kwa mujibu
wa maelezo ya mwanamke huyo ambaye alionekana kuwa msemaji wa familia
hiyo, yeye na mumewe mkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita,
wakitoka kijiji cha Usumbwa mpakani mwa Chunya, Mbeya na Tabora.
Wakiwa
kijijini hapo mume wake aliendelea kufanya kazi ya ukulima wakati yeye
mama (Veronica), pamoja na kilimo hujihusisha na upishi na uuzaji wa
pombe ya kienyeji iitwayo kayoga.
Mwanamke
huyo ambaye amesema ana watoto wanne, Alfred (20), binti mwenye miaka
16 (ambaye ameolewa) na wengine wawili wa kiume, mmoja akisoma darasa la
sita na mdogo ana miaka saba, amesema hana shida na waume wake.
Ingawa
wanandoa hao walizungumza kwa hadhari, majirani walikiri kuwa mwanamke
huyo anaishi na wanaume hao wawili kwa amani na kwamba mwanamke huyo
ndiye mwenye sauti na si waume zake.
“Si
siri tena sasa, tumeshawazoea, kwani wanaishi kwa amani ila yule mume
mdogo anaishi kwenye nyumba aliyoachiwa na marehemu baba yake, lakini
anashinda kwa mume mkubwa, ambapo inajulikana kijijini hapa kuwa ni
nyumba kubwa. “Basi pale ni mambo yote, kula na kunywa, mama huyu
amewapangia zamu wanaume hao kama afanyavyo mume mwenye wake wengi.
Ama
kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni,” alisema mkazi mmoja kwa
masharti ya jina lake kutoandikwa gazetini. Ilielezwa, kwamba wanaume
hao wana akili timamu na hawatumii kilevi cha pombe kama ilivyo kwa mke
wao.
Hata
hivyo, mume mkubwa anapewa sifa za upole tofauti na mume mdogo
anayetajwa kuwa mkorofi kiasi cha mara kadhaa kumchapa makofi mkewe
anapomuudhi.
Majirani
wanadai kwamba Mama Kaela na mumewe Paulo, walipofika kijijini hapo,
walipokewa na kuishi maisha ya kawaida, lakini baadaye mama huyo alianza
kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Arcado, ambaye naye alilazimika
kuachana na mkewe wa ndoa anayefahamika kijijini hapo kwa jina la Mama
Pere.
Ilielezwa
na mashuhuda hao kwamba mume mkubwa alipobaini uhusiano huo, alikuja
juu, lakini mwanamke huyo inadaiwa alimweleza mumewe huyo, atake asitake
lazima wataishi wawili, vinginevyo ataachana naye, ndipo mume mkubwa
alipokubali kuishi na mume mwenza.
Katika
maisha ya kawaida katika familia hiyo, inaelezwa kwamba katika baadhi
ya siku ikitokea kuwa mama huyo amechoka kupika, mume mdogo huchukua
jukumu la kupika na kumwandalia chakula na maji ya kuoga mume mkubwa.
“Lakini
mara nyingi kwa mfano, ikiwa ni zamu ya mama huyo kulala kwa mumewe
mkubwa, basi humfulia nguo zake kisha anakwenda kwa mumewe mdogo nako
anamfulia nguo.
MICHUZI BLOG
No comments:
Post a Comment