Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni
Dokta Gunini Kamba (katikati) akiwa na mratibu wa shindano la Redd's
Miss Kinondoni 2013, Ssebo wakitoa maelekezo kwa warembo mara baada ya
warembo hao kutembelea hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kutembelea
wagonjwa na kufanya usafi.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni
Dokta Gunini Kamba (kulia) akiwagawia warembo vifaa kwa ajili ya
kujikinga na vumbi mara baada ya warembo hao kutembelea hospitali ya
Mwananyamala kwa ajili ya kutembelea wagonjwa na kufanya usafi.
Warembo wajielekezana namna ya kuvaa vifaa vya kujikinga na vumbi kabla hawajaanza zoezi la kufanya usafi.
Mganga
Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dokta Gunini Kamba (kulia) akiwa na
mratibu wa shindano la Redd's Miss Kinondoni 2013, Ssebo wakiwaongoza
warembo mara baada ya warembo hao kutembelea hospitali ya Mwananyamala
kwa ajili ya kutembelea wagonjwa na kufanya usafi.
Mratibu wa shindano la Redd's Miss
Kinondoni 2013, Ssebo akiwaongoza warembo kuchukua vifaa kwa ajili ya
kuanza zoezi la kufanya usafi.
Warembo wa Redd's Miss Kinondoni 2013 wakiwa katika zoezi la kufanya usafi.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dokta Gunini Kamba (kulia) akiongea na vyombo vya habari.
Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2012/13 ambaye alitokea Redd'd Miss Kinondoni 2012 akiongea na vyombo vya habari.
Mratibu wa shindano la Redd's Miss
Kinondoni 2013, Ssebo akiongea na vyombo vya habari mara baada ya
kumalizika zoezi la kufanya usafi.
Bw. Ssebo alisema kuwa mchakato wa
kumtafuta Redd's Miss Kinondoni umeanza kwa kishindo ambapo warembo hao
ambao walishaanza kambi tokea mwishoni mwa wiki iliyopita jana waliweza
kutembelea hospitali ya Mwananyamala na kufanya usafi.
Warembo hao ambao wanajumuisha
vitongoji vya Dar Indian Ocean, Sinza na Ubungo baada ya kufanya usafi
hospitalini hapo walijionea hali mbaya iliyokuwepo pale na kuamua
kufanya harambee ya kuchangisha hela kwa ajili ya kununua vitanda kwa
ajili ya akina mama wanaojifungua (delivery beds).
Harambee hiyo imepangwa kufanyika
siku ya alhamis tarehe 13, katika ukumbi wa Ambassador kuanzia saa moja
jioni huku mgeni rasmi akiwa ni meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph
Mwenda.
Warembo hao leo watafanya usafi hospitali ya Sinza na kutembelea mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi.
Mashindano ya Redd's Miss Kinondoni
yanatarajiwa kufanyika June 21, huku walowa yamedhaminiwa na Redd's
Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products,
Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa
Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, Mrokim Blog 'FATHER KIDEVU BLOG',
SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog,
DjChoka Blog na Kajunason Blog.
No comments:
Post a Comment