Rais Barack Obama amewasili Senegal katika ziara yake
ya wiki moja barani Afrika na anatarajia kuzuru Afrika Kusini na
Tanzania akilenga kustawisha demokrasia na masuala ya uchumi.
Hii ni ziara ya pili ya Obama barani Afrika tangu achaguliwe Rais mwaka 2008.
Hii ni ziara ya pili ya Obama barani Afrika tangu achaguliwe Rais mwaka 2008.
Hata hivyo ziara yake inatarajiwa kufifishwa na
hali mbaya ya afya inayomkabili aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson
Mandela. Ikulu ya white house imesema kuwa itategemea uamuzi wa familia
ya Bwana Mandela iwapo Rais Obama anaweza kumtembelea hospitalini.
Katika mkutano wake wa leo na rais wa nchi hiyo,
Mackey Sall, Rais Obama anatajiriwa kuipa heko Senegal kwa rekodi yake
nzuri ya uthabiti ikizingatiwa iko kwenya kanda yenya misukosuko ya
kisiasa.
Maafisa wa Marekani wanasema kuwa muhimu katika
ziara ya Obama ni kustawisha demokarsia na nchi zote tatu anazotembelea
ziko na demokasria thabiti.
Ni ziara ya pili ya Obama katika bara la Afrika tangu kuwa rais wa Marekani mwaka 2008.
No comments:
Post a Comment