Redd's Miss Mwanza 2013, Lucy Charles akipozi kwa picha mara baada ya kuvikwa taji hilo.
Kinyanganyiro cha kumtafuta
mnyange wa mkoa wa Mwanza kwa mwaka 2013, kiliteguliwa usiku wa ijumaa baada ya
Mrembo Lucy Charles msomi wa chuo kikuu cha mtakatifu Augustino, kuwabwaga
warembo wengine 13 waliojitokeza.
Nyota ya mrembo huyo ilianza
kuonekana mapema, katika mavazi yote aliyovaa, lakini zaidi aliwapagawisha
mashabiki wa urembo waliofurika katika ukumbi wa Yatch club baada ya kujibu
swali kwa ustadi lililouliza Ni changamoto ipi kubwa walionayo vijana wa leo.
Mshindi wa pili katika
shindano hilo ni Judith Josephat na mshindi wa tatu ni Suzan Ikombe.
Washindi hao watawakilisha
mkoa wa mwanza katika shindano la kanda mwishoni mwa mwezi huu.
Redd's
Miss Mwanza 2013 Lucy Charles (katikati), akiwa katika picha ya pamoja
na mshindi wa pili Judith (kushoto) pamoja na mshindi wa tatu Suzan
Ikombe.
Vazi la Ubunifu
Kivazi cha Ufukweni
No comments:
Post a Comment