Katika kusheherekea maadhimisho ya miaka 30 legendari Hip -Hop studio Def Jam Recordings ilifanya tamasha moja la kukata na shoka katika ukumbi mashuhuri wa Barclays Center juzi usiku.
wasanii wote wa zamani na wapya walijumuika kwa pamoja kama vile kina Rick Ross, 2 Chainz, DMX, Fabolous , Foxy Brown, Jhené Aiko , Onyx, Method Man , Redman, Ashanti, Ja Rule , Warren G, EPMD na Jeremih .
Jambo ambalo lilionekana kuwafurahisha wapenzi wengi ni pale msanii mkongwe wa hip-hop Ja Rule alipompandisha juu ya jukwaa Ashanti na kuimba kwa pamoja zile njimbo zao classics ikiwa ni pamoja Mesmerize ' na ' always On Time' DMX nae alimkaribisha Swizz Beatz kuturudisha nyuma kwenye ile miaka ya 90 na nyimbo kali za Ruff Ryders.
Angalia Footage za baadhi ya tukio hilo hapo chini
No comments:
Post a Comment