Msanii mkongwe wa filamu za vichekesho nchini, King Majuto amesema
hivi kariburi alimshawishi Wema Sepetu azungumze na mpenzi wake Diamond
Platnumz ili wafanye kazi ya pamoja.
Mzee Majuto ambaye ni mshindi wa Tuzo za Watu 2014 ya filamu
inayopenda, ameiambia Bongo5 kuwa amemwachia kazi hiyo Wema ili
azungumzee na mzee (Diamond).
“Hivi karibuni nilikuwa na Wema, nimemwambia aongee na Diamond ili
tufanye filamu ya pamoja,” amesema Majuto. “Mimi, Wema na Diamond, hata
Diamond ninaweza kuzungumza naye sema nimeanza na Wema kwanza, akikubali
mtasikia tu.”
Kwa upande mwingine Majuto amesema ili acheze filamu anahitaji kulipwa shilingi milioni 3.
“Umri unaenda sasa biashara za nisaidie nisaide hakuna, kama unanitaka ili tufanye kazi unatakiwa uandae milioni 3.”
No comments:
Post a Comment