Maandandalizi ya tamasha kubwa la utamaduni wa mshwahili, Swahili
Carnical yanendelea vizuri baada ya wasanii wa muziki kuendekea
kuongezeka siku hadi siku.
Kati ya wasanii ambao watatoa burudani
siku ya tamasha hilo litakalolofanyika kwenye viwanja vya Posta
Kijitonyama jijini Dar es Salaama ni pamoja na mkali wa muziki wa Taarb
nchini, Isha Mashauzi akiwa na bendi yake ya Mashauzi Clasic.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam Mratibu wa tamasha hilo la siku tatu, Ahadi Kakore
alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na kwamba Isha ni miongoni
mwa wasanii wa taarab ambao watakata kiu ya wapenzi wa muziki Tanzania
hasa muziki wa taarab.
"Tunashukuru Mungu kwamba kila kitu kinakwenda sawa licha ya changamoto zilizopo lakini tunaendelea mbele.
"Kwa
upande wa burudani tumeweza kufanikiwa kumalilisha kumpaga gwiji wa
muziki wa taarab Tanzania, Isha Mashauzi ambaye ataungana na bendi
nyingine ikiwemo Yamoto Band katika kuhakikisha watakaokuwepo kwenye
tamasha hilo wanapata burudani mwanzo mwisho," alisema Kakore.
Burudani
zitakazokuwepo kwenye tamasha hilo ni moja na muziki, mchezo wa soka
kwa madiwani, michezo ya jadi, filamu za Kiswahili, maonyesho ya
mavazi, bidhaa za Wajasiliamali na michezo ya watoto.
Tamasha la
Swahili Carnival litafanyika kuanzia Novemba 28 hadi 30 kwenye viwanja
vya Posta jijini Dar es Salaam ambapo milango itakuywa wazi kuanzia saa
3:00 asubuhi hadi saa 7:00 mchana.
No comments:
Post a Comment