Baba
wa Edina Julis (10) akiwa amembeba mtoto wake mwenye maumivu makali ya
mguu wakirundi nyumbani baada ya kukosa huduma leo katika hospitali ya
Bugando...hata hivyo baadhi ya wauguzi wa kliniki ya mifupa wamemshauri
baba huyo kumpeleka mtoto wake katika hospitali binafsi baada ya kuhisi
huenda tatizo la mtoto huyo kuwa kubwa kama atakaa bila yaa kupata
huduma. Yaliyojiri
leo Hospitali ya rufaa Bugando jijini Mwanza mgomo upo tena unafukuta
chini kwa chini na memo tayari zimebandikwa kwenye baadhi ya milango ya
vyumba vya mikutano ya wanataaluma wa utibabu tangu jana, Uongozi
unakigugumizi kulizungumzia hili na kuweka bayana. Tangazo
linasema:-Kuanzia leo tarehe 7/2/2012 siku ya jumanne saa sita mchana
tunataarifu kuwa tunasitisha huduma zote zikiwemo zile za dharula hadi
hapo serikali itakapotimiza madai yote yanayosimamiwa na kamati kuu ya
madaktari Tanzania. Imetolewa na jumuiya ya Madaktari bugando
(Residents, Registrers,Interns) Huku
akipinga kauli iliyoripotiwa na baadhi ya Vyombo vya habari kuhusu yeye
kuagiza wagonjwa kuja toka mikoa mbalimbali nchini kuja kupata huduma
hospitalini hapa, Kaimu mkurugenzi wa Hospitali ya Bugando Dr.Japhet
Giliyoma hakuwa tayari kuelezea bayana hali halisi akisisitiza kuwa mkuu
wa mkoa ndiye atakayetoa taarifa rasmi kwani tayari wamekwisha mpatia
hali halisi. Mapokezi wagonjwa wengi wamelalamikia suala la kupigwa tarehe kurejea wiki kadhaa zijazo... "Naitwa
Rehema Wasongwa tareha 25 nilikuja wakanipa tarehe ya leo, leo nimekuja
wamenipiga tarehe wiki mbili kurudi tena mimi masikini nitafanyaje na
ninasafiri kutoka Musoma hadi Mwanza kuitafuta huduma?" Julius
Lutabi baba wa mtoto Edna aliyegongwa na gari toka jumamosi iliyopita,
yuko hapa tangu asubuhi jibu limetoka akipigwa tarehe mpaka.... ameiomba
serikali kusitisha mijadala mingine na kuigeukia wizara ya afya. Mwendo ni kupigwa karenda tuu wengi wamekosa huduma...
No comments:
Post a Comment