TWANGA PEPETA BADO WAMO, WASUGUA VISIGINO MWANZO MWISHO USIKU WA WAPENDANAO (VALENTINE DAY) EQUATOR GRILL
Mwimbaji
wa bendi ya African Stars Janet Isinika kushoto akicheza pamoja na
wanenguaji wa bendi hiyo katika onyesho la usiku wa wapendanao Valentine
Day lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Equator Grill
Mtoni kwa Azizi Ali jijini Dar es salaam, Wapendanao walijumuika na
wapenzi wao kusherehekea siku hiyo ambayo imekuwa ikijichukulia umaarufu
siku hadi siku hapa nchini Tanzania.
Asha
Baraka Mkurugenzi wa African Stars akiongea na wadau wa bendi hiyo
wakati wa onyesho la bendi yake usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa
Equator Grill Mtoni kwa Azizi.
Hii ni staili ya kulia na kubembelezwa kutoka kwa wana wa Kutwanga na Kupepeta African Stars.
Janet Isinika akicheza na mmoja wa wa wanenguaji wa kiume wa bendi ya African Stars.
Mdau
Mohamed Jumakushoto akiwa na rafiki yake Muhsin nao walikuwepo
kuwashuhudia wana wa Kutwanga na Kupepeta katika usiku wa wapendanao
usiku wa kuamkia leo.
Wapenzi
wa bendi ya African Stars wakijimwaga kusakata rhumba ukumbini wakati
bendi hiyo ilipokuwa ikifanya vitu vyake usiku wa kuamkia leo.
Vimwana
wa bendi ya Africana Stars wakionyesha ujuzi wao jukwaani wakati bendi
yao ilipokuwa ikifanya vitu vyake kwenye ukumbi wa Equator Grill usiku
wa kuamkia leo jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment