UMOJA
wa Afrika (AU) umemteua Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa nchini (Takukuru), Dk Edward Hosea kuongoza Secretarieti ya Bodi
ya Kuzuia Rushwa Barani Afrika.AU pia imeteua makao makuu ya
Sekreterieti hiyo kuwa mjini Arusha, ambapo shughuli zake zote
zitaratibiwa. Akizungumzia
kuhusu uteuzi huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bernard Membe alisema ulifanywa na AU katika mkutano wake uliomalizika
hivi karibuni mjini Addis Abba, Ethiopia. Alipoulizwa
mambo yaliyoifanya Dk Hossea na Tanzania kupata heshima hiyo wakati
ambapo Taifa limekuwa likikabiliwa na misuguano ya rushwa, Membe
alisema: “Uhuru
huo wa kuruhusu mijadala ya rushwa nchini ndiyo yanayoijengea heshima
Tanzania. Hii inaonyesha uwazi wa mapambano dhidi ya rushwa.”Alisema
kwamba rushwa ipo sehemu nyingi duniani lakini ni nchi chache zinazotoa
uhuru wa wa kuzungumza mambo hayo hadharani kama ilivyo Tanzania. “Vyombo
vya habari vimekuwa huru... Kuwepo kwa mijadala, misuguano, kunatoa
fursa ya kuweka sera na mipango ya kukabiliana na rushwa,” alisema
Membe. Katika
hatua nyingine Membe alisema kwamba AU imeshindwa kumchagua Katibu Mkuu
wa Umoja huo baada ya aliyekuwa anatetea nafasi hiyo, Jean Ping wa
Gabon kukataliwa kwa kura. Membe
alisema uchaguzi huo sasa utafanyika Julai mwaka huu mjini Lilongwe,
Malawi na kuna uwezekano mkubwa wa katibu mpya kutoka katika nchi za
Kusini mwa Afrika.Wakati huo huo, Membe alisema kwamba AU imekasirishwa
na kitendo cha Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kuwaandama
viongozi wa Afrika peke yao, huku wakiwaaacha wa mabara
mengine.Kutokana na hali hiyo wametaka ICC ifanyiwe marekebisho ili
iweze kuendesha shughuli zake kwa haki duniani.
No comments:
Post a Comment