Kamanda
wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow akikabidhiwa rasmi
mchango wa matairi 50 yaliyotolewa asubuhi ya leo na mfanyabiashara
maarufu Zuri Nanji kwaajili ya makarandinga ya jeshi hilo.
Mfanyabiashara
Zuri Nanji amesema kuwa msaada huo ni kielelezo tosha cha utendaji bora
wa jeshi la polisi Mwanza na amesihi jeshi hilo kuendeleza sera yake ya
ulinzi shirikishi.
Kamanda Barlow akikagua umadhubuti wa matairi hayo yenye jumla ya thamani ya shilingi milioni 20.
Sehemu ya maafisa wa jeshi la polisi walioshiriki makabidhiano hayo yaliyofanyika mbele ya ofisi za jeshi la polisi Mwanza.
Mfanyabiashara
maarufu Josephat Musukuma (anayezungumza) alitoa shilingi milioni moja
kwaajili ya mfuko wa magari ya doria ambayo yamekuwa yakikumbwa na
kadhia ya kukwama kufika sehemu za matukio kutokana na uhaba wa mafuta
sambamba naye Mfanyabiashara Riziki Mbise wa Kampuni ya Mambo ya Chinga
Investiment (katikati) akikabidhi mchango wake wa milioni moja taslimu
kwa katibu wake wa mfuko wa wafanyabiashara kwenda kwa jeshi la polisi.
Kamanda wa kikosi cha Doria na Ulinzi shirikishi Philip Karage akitoa shukurani kwa mchango huo.
'KITU KASHATA MMmma' ni karandinga lililofungwa tairi zote mpya.
Naye
mfanyabiasha Rashid alitoa lita 400 za mafuta kwaajili ya vyombo vya
doria, msaada huo utalinusuru jeshi la polisi na aibu ya makarandinga
yake na pancha za mara kwa mara wakati wa safari zake pamoja na kukwama
kutokana na uhaba wa mafuta.
No comments:
Post a Comment