
BODI YA TAIFA YAFUTA MISS UTALII KANDA YA ZIWA 2012
Bodi ya Taifa ya Miss Tourism Tanzania Organisation (MTTO),imefuta na
 kutokulitambua shindano la Miss Utalii Kanda ya Ziwa 2012 lililo 
fanyika New Mwanza Hotel ,wakati taifa likiwa katika maombolezo ya msiba
 mkubwa wa kitaifa wa watu waliopoteza maisha katika ajali ya meli iliyo
 tokea Zanzibar.
Bodi imechukua hatua ya kulifuta na kutolitambua shindano hilo, 
ambalo limefanyika bila ya kuzingatia misingi ya kibinadamu na hata 
uzalendo kwa Taifa. Waandaaji wa shindano hilo Fania Hassan wa Fania 
Beauty Salon,pamoja na kutambua kuwa taifa lipo katika maombolezo ya 
siku tatu kwa tangazo na tamko la serikali, bado hakuzingatia maelekezo 
ya waandaaji wa Taifa ambao walisitisha mashindano ya Miss Utalii 
Tanzania katika ngazi zote,likiwemo lile la Miss Utalii Kinondoni 2012 
ambalo lilikuwa lifanyike tarehe 20-7-2012 katika ukumbi wa Traveltine 
Dar es Salaam ambalo sasa litafanyika 31-7-2012 katika ukumbi wa Club 
Maisha Oyterbay na lile la Miss Utalii Ilala 2012 ambalo lilikuwa 
lifanyike 21 -7-2012 katika ukumbi wa Eriado View pont Pugu Dar es 
Salaam ambalo sasa lifanyika siku ya Iddy Pili katika ukumbi wa Eriado 
point View Pugu.
Bodi ya mashindano katiaka kikao chake cha dharula kilichofanyika leo
 asubuhi baada ya kupata taarifa kutoka kwa vyanzo vyetu vya uhakika,juu
 ya kufanyika kimyakimya kwa shindano hilo imeamua kuchukua hatua hiyo 
kali ya kulifuta na kutolitambua shindano hilo, ili iwe fundisho kwa 
waandaaji wengine wasiozingatia maagizo kwa mujibu wa kanuni na taratibu
 za mashindano haya. 
Bodi imesikitishwa sana na tukio hilo kisilo la kizalendo, na 
inawaomba radhi watanzania wote,ndugu na jamaa wote waliopoteza ndugu 
zao katika ajali hiyo,serikali, mamlaka zote za mkoa wa Mwanza, mamlaka 
za sanaa,wadhamini na wadau mbalimbali wa mashindano ya urembo utalii na
 utamaduni nchini na nje ya nchi.
Washiriki wote watalazimika kusubiri tarehe mpya ya kufanyika kwa 
shindano hilo,baada ya mfungo wa ramadhani,ambapo pia watagharamiwa 
gharama zote za ushiriki wao upya,kama kanuni na taratibu za mashindano 
zinavyo bainisha kuwa washiriki wote wa mashindano ya Miss Utalii 
tanzania wanagharamiwa gharama zote za mavazi,usafiri,vinywaji,chakula 
na saluni.
Kamati ya nidhamu ya mashindano haya itakutana mwisho wa mwezi ili 
kujadili hatua zaidi za kuchukua dhidi ya waandaaji hao wa Miss Utalii 
kanda ya Ziwa 2012.
Haiwezekani hata kidogo wakati taifa lina omboleza halafu mtu 
anatumia mashindano haya ambayo ni alama ya urithi wa Taifa na kielelezo
 cha utamaduni wa mtanzania kukiuka utamaduni,mila na desturi za 
Tanzania,tena wakati hata serikali 
imetangaza maombolezo na bendera zinapepea nusu mlingoti. 
Kwa mara nyingine tena tunaungana na watanzania wote kuwapa pole 
Ndugu zetu wa Zanzibar walio Potelewa na ndugu jamaa pamoja na Marafiki,
 Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape Nguvu katika kipindi hiki kigumu. 
Pia kwa wale majeruhi na ambao wapo kwa matibabu pia Tunawaombea wapate 
kupona Haraka ili warejee katika kazi zao za kujenga taifa. 
Miss Utalii Tanzania ni Alama ya Urithi wa Taifa – Utalii ni Maisha ,Utamaduni ni Uhai wa Taifa.
Asante,
Abubakari Omary Bakari
MKURUGENZI WA UTAWALA NA FEDHA - MISS TOURISM TANZANIA ORGANISATION
No comments:
Post a Comment