Miss
Morogoro 2012 Joyce Baluhi (katikati) akiwa na washindi wenzake,
Salvina Kibona mshindi namba mbili (kushoto) na Irene Thomas mshindi
namba tatu mara baada ya kumalizika kwa shindano la Miss Morogoro
lililofanyika katika ukumbi wa Morogoro Hoteli mwishoni mwa wiki.
Miss Moro Morogoro 2012 Joyce Baluhi kushoto akiwa na Miss Morogoro 20111, Asha Salehe kulia mara baada ya kumkabidhi taji hilo.
Mgeni
rasmi shindano la Miss Morogoro 2012 ambaye ni Afisa Mwendeshaji wa
mfuko wa pensheni kanda ya mashariki na kati (PPF) Astronaut Liganga
kulia liyesimama akiwa katika picha ya pamoja na Miss Morogoro 2012,
Joyce Baluhi aliyekaa, Mratibu wa shindano hilo Frank Kikambako kushoto
aliyesimama na warembo wengine walioingia tano bora mara baada ya
kutangazwa matokeo na kuwapata washindi.
Hawa
ndiyo warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bara kutoka na
kuchujwa kupata mshindi wa kwanza, pili na tatu ambao warembo hao
watashiriki shindano la Miss Kanda ya Mashariki.
Picha
ya pamoja ya washiriki wote 13 ambao walishiriki shindano hilo baada
ya kupanda kujukwaani na vazi la ubunifu, ufukweni na jioni katika
kinyang'anyiro hicho.
mrembu naye akiwa katika vazi la ubunifu.
Mrembo Prisca Mengi (18) akipita mbele ya majaji na mashaki na vazi la ubunifu.
Rais wa bende ya FM Academia (wazee
wa Ngwasuma), Nyoshi El- Saadat akiimba wakati bende yake ikitumbuiza
mashabiki waliohudhuria shindano hilo ndani ya viwanja vya wazi vya
hoteli ya Morogoro.
Mmoja wa wanenguaji wa bendi ya FM Adademia akicheza kwa aina mpya kwa staili ya Vundesa.
JOYCE
Baluhi (22) ameibuka katika shindano la kumsaka Miss Morogoro 2012
baada ya kutwaa taji hilo lililokuwa na ushindani wa hali ya juu
lililofanyika kwenye viwanja vya wazi vya hoteli ya Morogoro mwishoni
wa wiki mkoani hapa.
Shindano hilo ambalo lilishirikisha warembe 13 ambapo Salvina Kibona (20) kwa kutwaa nafasi ya pili wakati nafasi ya tatu ikichukuliwa na Irene Thomas (20) ambao walifanikiwa kuvuka katika hatua ya tano bora.
Shindano hilo ambalo lilishirikisha warembe 13 ambapo Salvina Kibona (20) kwa kutwaa nafasi ya pili wakati nafasi ya tatu ikichukuliwa na Irene Thomas (20) ambao walifanikiwa kuvuka katika hatua ya tano bora.
Dalili
za Baluhi kutwaa kwa taji hilo zilionekana mapema hasa katika onyesho
la vazi la ubunifu, ufukweni na jioni kabla ya kumalizia kizingiti cha
mawaswali na kuibua shngwe na ndelemo kutoka kwa mashabiki
waliohudhuria shindano hilo kwa kila hatua ambayo akionekana mlimbwende
huyu baada ya kulitawala jukwaa.
Katika
shindano hilo ambalo lilisindikizwa na bendi ya muziki wa dansi ya
bende ya FM Academia (wazee wa Ngwasuma) chini ya Rais wao, Nyoshi El-
Saadat lilikonga nyoyo za wapenzi wa dansi na shindano hilo ambapo
walitumbuiza nyimbo mbalimbali zilizopo katika chati hivi sasa.
Mwandaaji
wa shindano hilo la Miss Moro 2012, Frank Kikambako alisema kuwa
mshindi wa kwanza amejipatia sh400,000 huku mshindi wa pili akipata
sh300,000 na mshindi wa tatu akipata zawadi ya sh250,000 na washiriki
wote walioshiriki shindano hilo wakiambulia pesa ya sh50,000 kila mmoja
kama kifuta jasho.
Naye
mgeni rasmi katika shindano hilo Afisa Mwendeshaji wa mfuko wa
pensheni kanda ya mashariki na kati (PPF), Astronaut Liganga alisema
kuwa warembo waliofanikiwa kuingia tano bora na hatimaye kumpata Miss
Moro 2012 ambao wote watashiriki shindano la Miss Kanda ya Mashariki
kuwa na nidhamu mzuri itayochangia na sifa nyingine kuvuka vikwazo
katika shindano hilo.
Aliwataja warembo ambao walifanikiwa kutinga hatua ya tano bora ni Nafya Waziri (19) na Betina Lawurence (20).
Liganga
alisema kuwa sifa pekee katika tasnia nyingi za michezo ikiwemo na
urembo ni kuwa na nidhamu mzuri na kuwataka washiriki wengi ambao
hawakupata nafasi ya kusonga mbele kuendeleza nidhamu walioionyesha
katika kambi ya Miss Morogoro.
No comments:
Post a Comment