Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu wa Zanzibar, Hamad Masoud (pichani) amejiuzulu kufuatia shinikizo za za watu na maandamano.
Kumekuwa
na msukumo kutoka kwa makundi mbali mbali ya kutaka waziri huyo
ang'atuke kufuatia kuongezeka kwa ajali za baharini kati Hatua hii
imekuja kufuatia madai ya wananchi kuwa ajali za meli zimekuwa
zikiongezeka mjini Zanzibar bila yeye kuchukua hatua yeyote.
Mbali
na kujiuzulu kwa Hamad kama Waziri, Rais wa Zanzibar Ali Mohammed Shein
ameunda Tume ya kuchunguza kiiina cha Meli hiyo ya MV Skagit kuzama na
kuuwa watu.
Mwenyekiti
wa tume hiyo atakuwa Jaji Abdulhakim Ameir Issa, wanachama watukiwa
Meja Jenerali S.S. Omar, Komanda Hassan Mussa Mzee, Kapteni Abdulla
Yussuf Jumbe, Kaptein Abdulla Juma Abdulla, Salum Taoufiq,Kaptein Hatibu
Katandula, Bi. Mkali Fauster Ngowo, Ali Omar Chengo na Shaaban Ramadhan
Abdalla Katibu wa Tume.
Kufuatia shinikizo hizo Siku ya Ijumaa ,tarehe 20 Julai ,Hamad Masoud alimuandikia barua rais wa Zanzibar kumuomba kujiuzu.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka chama tawala cha CCM, Rais wa Zanzibar Ali
Mohammed Shein amekubali ombi la Waziri Hamad Masoud kujiuzulu.
Kufuatia
kujiuzulu kwa waziri huyo, Rais ,Dk Shein amemteua Mbunge wa Jimbo la
Ziwani Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri mpya wa Miundombinu na
Mawasiliano.
Taarifa kutoka ikulu zinasemna kuwa uteuzi wa Bwana Rashid Seif Suleimna utaanza mara moja
No comments:
Post a Comment