Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Sunday, October 13, 2013

MIMBA YA ROSE NDAUKA YAWA GUMZO KATIKA BDAY YAKE

 
MUONEKANO mpya wa ‘kubugia kijusi’ wa msanii wa filamu za Kibongo, Rose Donatus Anjelus Ndauka ‘mtata’ umezua miguno, minong’ono huku ikionekana kivutio kwa wengi na kubaki wakihoji maswali yasiyojibika haraka.
Hayo yalichukua nafasi hivi karibuni wakati staa huyo alipofanya sherehe ya kutimiza miaka kadhaa tangu ‘anuse hewa ya Oksijeni’ iliyofanyika ndani ya ukumbi wa Club Escape Beach Kigamboni jijini Dar na kuacha historia ya aina yake.
  Baadhi ya wahudhuriaji wa sherehe hiyo, walionekana kuwa na viulizo vingi juu ya mimba yake, huku gauni fupi alilovaa siku hiyo likiionesha kwa ufasaha mimba hiyo na kufanya baadhi yao kubaki wasiamini kama kweli msanii huyo amechukua uamuzi wa kuzaa kabla ya ndoa.
“Mh! hivi kweli Rose ana mimba?, siamini kama ameamua kuzaa kabla ya ndoa si alikuwa akikataa huyu? Sasa imekuwaje” alisikika mama mmoja katika sherehe hiyo.
“Ila kapendeza jamani, sasa kaonekana mwanamke kweli,  muone anavyotembea kwa madaha, mimba hiyo imemuongezea mvuto!” alisema msanii mwingine wa kike mwenye ‘taito’ kubwa bongo.
Mwandishi wetu alipomuuliza Rose juu ya minong’ono hiyo, alijibu kwa kifupi huku akionekana kufurahia.
“Jamani sina jibu la kuwapa, kama watu wanashangaa ni wao niseme nini tena?” alisema Rose na kisha kufunga ‘faili’ la mazungumzo na mwandishi wetu.

No comments: