Askari
wa uhamiaji wamewakamata watu 14 katika maeneo ya Msasani jijini Dar es
Salaam kutoka nchini India na Nepal ambao ni wahanga wa biashara haramu
ya usafirishaji wa binadamu ambapo watu hao wameingia nchini kinyume na
taratibu za uhamiaji.
Kati
ya watuhumiwa 14 watuhumiwa 12 ni wasichana ambao waliletwa nchini kwa
lengo la kufanya maonyesho ya nyimbo za asili lakini wakajikuta
wakingizwa katika biashara zingine ikiwemo kucheza muziki katika nyumba
za burudani.
Kwa
upande mtu anayedaiwa kuwaleta wasichana hao amesema amewaleta kwa
lengo la kufanya maonyesho ya muziki huku akipinga kuwa wasichana hao
hawatumii kinyume na hivyo.
Naye
mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa mikoroshini msasani amewataka wakazi
wa eneo hilo kujiepusha na tabia ya kukaa na wageni bila ya kutoa
taarifa mamlaka husika.
Akithibitisha
tukio hilo mkaguzi wa uhamiaji Bw Dotto Romana amesema wanawashikilia
watu hao na watachukua hatua kulingana na mahitaji ya sheria.
No comments:
Post a Comment