Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Thursday, September 25, 2014

Said Fella aelezea jinsi alivyosaka mchongo wa Shaa kulipwa kupitia YouTube

 Video: Said Fella aelezea jinsi alivyosaka mchongo wa Shaa kulipwa kupitia YouTube
Meneja mkongwe na muewezeshaji wa Mkubwa na Wanae, Said Fella amefunguka kuhusu njia alizotumia kutafuta nafasi ya biashara ya wasanii wake akiwemo ‘Shaa’ kulipwa pale kazi zake zinapowekwa YouTube.
Akiongea na tovuti ya Times Fm, Fella amesema yeye na Babu Tale waliumiza kichwa baada ya kuona wasanii wa Kenya wanaingiza pesa hata kama hawajatoa wimbo mpya, bila kutegemea shows na ndipo walipoamua kusafiri hadi Nairobi kuhakikisha wanafahamu nini hasa cha kufanya.
“Kweli tukaenda Kenya, tukaenda kukutana watu tukawauliza ‘jamani nyie mnaendaje mbona sisi tukiwapelekea wenzetu wanaotuuzia ringtone hapa Tanzania hatupati faida ile’. Lakini unakuta Jua Cali au Nyota Ndogo kafanya muziki zamani lakini anaendelea kula faida.” Amesema Said Fella.

“Yaani tumesafiria tobo na ndio maana tumelipata tobo. Hata juzi kati Babu Tale na Diamond walivyoenda Nigeria kwenda kusaka tobo…na ndio maana tunasema timu yetu Saka Tobo ili kwenda kuangalia wenzetu wanafanya nini na tunakwenda wapi. Kwa hiyo huwezi kumfuata tu mtu ukamwambia ebwana tobo hili…waje tuwaoneshe. Watanzania tunapendana.” Said Fella ameiambia tovuti ya Times Fm.
Shaa ambaye kimuziki anasimamiwa na Said Fella hivi sasa analipwa kwa kazi anazoweka kwenye channel ya YouTube.
Video yake ‘Sugua Gaga’ imevunja rekodi ya video za bongo flava kwa kuangaliwa zaidi YouTube, hadi leo imeangaliwa zaidi ya mara 4,656,000.

No comments: