Mwisho wa siku wananchi haoooo...warejea makwao kwa amani na utulivu hakuna aliyeumia wala kupigwa kwenzi licha ya umati kufurika katika maandaamano na uwanjani Furahisha.
Chama cha maendeleo na demokrasia nchini CHADEMA leo kimefanya maandamano ya amani katika jiji la Mwanza kupinga kupinga mchakato wa uchaguzi na matokeo ya Meya wa Jiji la Arusha, kuunga mkono maandamano yaliyofanywa na chama hicho mkoani Arusha Januari 5, mwaka huu na kupinga zoezi la serikali kulipa deni la Dowans.Maelfu ya wakazi wa jiji la Miamba muda huu wamejitokeza kwa wingi kuliunga mkono zoezi hili ambalo limeanzia eneo la Buzuruga wilaya ya nyamagana na kuelekea katika viwanja vya Furahisha wilayani Ilemela ambapo kutakuwa na mkutano.
MabangozZZZ!!..
Hali ya hewa barabara ya Kenyeta.
Mmiliki wa dowans aka.....
Barabara ya Makongoro kuelekea kata ya Kirumba uwanja wa Furahisha eneo ambako mkutano utafanyika jioni ya leo.
Ujumbe kwa wakazi wa Gongo la mboto toka CHADEMA Mwanza.
Pikipiki eneo la kipita shoto cha ilipokuwa sanamu ya baba wa taifa.
MabangozZZZ!!..
Hali ya hewa barabara ya Kenyeta.
Mmiliki wa dowans aka.....
Barabara ya Makongoro kuelekea kata ya Kirumba uwanja wa Furahisha eneo ambako mkutano utafanyika jioni ya leo.
Ujumbe kwa wakazi wa Gongo la mboto toka CHADEMA Mwanza.
Pikipiki eneo la kipita shoto cha ilipokuwa sanamu ya baba wa taifa.
(PICHA NA;gsengo)
MUSTAFAH KUJA NA MPYA
Mustafa Hassanali addresses a safe motherhood campaign during press conference held at Habari Maelezo today, right is Ms Rose Mlay, the country coordinator of White Ribbon Alliance and Safe Motherhood in Tanzania.
Yale maonyesho ya mavazi yajulikanayo kama ‘mamma mia’ yenye nia ya kuhamasisha uzazi salama, sambamba na sherehe za miaka 50 ya uhuru Tanzania, na miaka mia moja ya siku ya mwanamke duniani , kwa kushirikiana na shiriki lisilo la kiserikali la utepe mweupe ‘White Ribbon Alliance’ na ‘Vodacom Foundation’, yazinduliwa rasmi.
Akizungumza katika uzinduzi huo, mbunifu wa mavazi, aliyejipatia umaarufu kitaifa na kimataifa, Mustafa Hassanali amesema “ntazindua toleo langu jipya la ki-afrika katika maonyesho haya ya ‘Mamma Mia’ siku ya tarehe 4 na tano mwezi Machi hapahapa jijini Dar es salaam, na nategemea kupata ushirikiano wa watu wote, katika kuhamasisha uzazi salama kwa msaada wa shirika la utepe mweupe”
‘Mamma Mia’ ni jukwaa la maonyesho ya mavazi ambalo limelengwa mahsusi katika kusambaza ujumbe kuhusu uzazi salama, litafanyika tarehe nne mwezi machi, katika hoteli ya ‘Moevenpick Royal Palm’ kuanzia saa mbili na nusu usiku, na onyesho jingine kwa siku ya Jumamosi ya tarehe tano kuanzia saa tisa na nusu jioni, katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Mapigano makali yanaarifiwa kutokea katika maeneo matatu nchini Somalia.
Mwaandishi wa BBC anasema haya ni mapigano makali kabisa kati ya majeshi ya serikali na wapiganaji wa kundi la wanaharakati wa kiislamu la Al-Shabab, katika mji mkuu, Mogadishu, katika kipindi cha miezi michache iliyopita.Vikosi vya serikali vikisaidiwa na wanajeshi wa Muungano wa Afrika, inasemekana vimeiteka ngome kuu ya al-Shabaab .
Kuna taarifa za kutokea mapambano katika mji wa Beledweyne kwenye mpaka wa Ethiopia na Bulahawa, na kwenye mpaka na Kenya.
Mapigano makali ya mjini Mogadishu yaliendelea siku nzima Jumatano.
Wanajeshi kutoka Burundi ambao ni sehemu ya jeshi la Muungano wa Afrika wamekuwa wakipigana bega kwa bega na wanajeshi wa serikali hiyo ya mpito ya Somalia.
Wamefanikiwa kuyateka maeneo ya wapiganaji wa Al Shabab baada ya kusonga mbele mtaa kwa mtaa.
Eneo liliotekwa ikiwemo iliyokuwa wizara ya ulinzi ni dogo lakini ni muhimu katika mikakati ya kijeshi.
Kundi la Al Shabab pia limekabiliwa na shinikizo katika mji wa Beledweyne kwenye mkoa wa kati wa Somalia ambako wanajeshi wa serikali na wanamgambo washirika wamekuwa wakifanya mashambulizi.
Katika medani ya tatu ya mapigano Bula Hawo karibu na mpaka wa Kenya wapiganaji wanaohusishwa na kundi la Al Qaeda walishambuliwa na kundi jingine la wanamgambo wanaoiunga mkono serikali.
Ingawa mpaka huo umefungwa rasmi , wakazi wamekuwa wakikimbia mapigano ya huko na kuelekea mji wa Mandera nchini Kenya.
Rais wa Somalia, Sheikh Sharif Sheikh Ahmed alihutubia waandishi wa habari mjini Mogadishu.
Akiwa amevalia sare ya kijeshi , aliwasifu wanajeshi wa serikali na kusisitiza kwamba mashambulio hayo katika maeneo tofauti yameratibiwa.
Jeshi la Muungano wa Afrika na wanajeshi wa serikali wanazungumzia kuendelea kulivunja nguvu kundi la Al Shabab, hata hivyo kundi hili la msimamo mkali wa kiislamu bado linadhibiti maeneo makubwa ya nchi na linaweza kusababisha vurugu kubwa.
Siku ya Jumatatu bomu liliotegwa ndani ya gari liliwaua watu wasiopungua 17 karibu na kituo cha mafunzo ya polisi mjini Mogadishu.
SHEKH YAHYA ATABIRI SERIKARI YA JK KUYUMBA
No comments:
Post a Comment