Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Thursday, February 17, 2011

MAJERUHI WA MABOMU WAONGEZEKA

ZANTEL YATOA MSAADA WA KATONI 100 ZA MAJI KWA WAHANGA


Baadhi ya Maofisa wa Kampuni ya simu Zantel wakishusha msaada walioutoa wa katoni 100 za maji Uwanja wa Uhuru kwa waasilika wa mabomu yaliyotokea kambi ya Jeshi Gongolamboto Dar es salaam.


KAMBI YA WAHANGA WA MABOMU YAHAMIA UWANJA WA UHURU JIJINI DAR 

Mama wa watoto wa tatu aliejitambulisha kwa jina la Zawadi Hassan akiwa na watoto wake wawili huku akihuzunika kwa kutokujua alipo mtoto wake mmoja wapo kutokana na kukimbia kwa kujinusuru na mabomu yaliyokuwa yakilipuka usiku wa kuamkia leo huko gongo la mboto.

Watoto wadogo wengine wakiwa hawana mashati toka usiku wa jana wakipita mbele ya umati kutambuliwa na ndugu na wazazi wao.
 Mtoto Gerald simon akiwa nachupa ya maji huku akiugulia majeraha katika kambi ya wahanga ambapo aliumia wakati aiokoa roho yake jana usiku.
Gongo la mboto swala kubeba watoto mgongoni ni zamu ya akina baba kuchunga watoto wao wasipotee,gender equality
Mibomu hii ikikupata mtu mzima mmhh si mchezo kuna haja ya kuhamisha kambi za jeshi kwenye makazi ya watu.
Ukuta wa numba ukiwa umegadhibishwa kisha kuvunjwa  na bomu lililolipuka jana usiku toka kambini hadi uraiani.



   'SIKU YA GADHABU' GHASIA ZAIBUKA- LIBYA

Watolewa na wanaharakati kupitia mitandao ya kijamii
Wanaharakati wanaopinga serikali nchini Libya wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kupata watu wa kuwaunga mkono kwenye maandamano ambapo wanaelezea kama "siku ya ghadhabu."
Kulikuwa na ripoti za mapigano katika miji miwili siku ya Jumatano, huku takriban watu wanne wakiripotiwa kufariki dunia katika mji wa al-Bayda mashariki mwa nchi hiyo.
Idadi kubwa ya watu walijeruhiwa katika maandamano yaliyo na vurugu siku ya Jumanne usiku katika mji wa Benghazi.
Ghasia hizo zimeibuka baada ya mkosoaji wa serikali kutiwa kizuizini.
Maandamano ya kuunga mkono demokrasia hivi karibuni yameenea katika mataifa ya kiarabu, huku marais wa Tunisia na Misri walipolazimika kujiuzulu kutokana na ghasia hizo.
Lakini maandamano ya wiki hii ni mara ya kwanza kuonyesha ujasiri wa kweli nchini Libya, nchi ambayo kupingwa hakustahamiliwi.

No comments: