Mwenekiti wa chama cha wananchi CUF Bwana Ibrahim Lipumba akibeba jujuu kiroba cha unga kutoka kwenye gari wakati chama hicho kikikabizi msada huo kwa wahanga wa mlipuko wa mabomu katika kambi ya jeshi Jwtz huko gongo la mboto leo.
WAPINZANI WALIPULIWA NIGERIA

Jimbo la Niger Delta nchini Nigeria
Kumetokea mlipuko mkubwa katika afisi za kampeni za chama cha upinzani nchini Nigeria katika jimbo la Bayelsa lililoko katika eneo la Niger Delta.
Mlipuko huo uliotokea mapema jana ulisababisha uharibifu katika jengo hilo, ambako chama cha upinzani cha Labour Party kina afisa zake.Hata hivyo hakuna ripoti zozote za majeruhi.

Uchaguzi mkuu utafanyika mwezi Aprili.
Mwezi uliopita magenge ya watu waliokuwa na silaha waliwauwa wafuasi wa chama hicho cha Labour katika mkutano wa kampeni.
Hata hivyo, msemaji wa serikali wa jimbo la Bayelsa amesema chama cha Labour Party ndicho kilicho tekeleza mashambulio hayo, ili kuvutia macho ya vyombo vya habari.
Uchaguzi wa urais, bunge na magavana utafanyika Aprili mwaka huu.
MAGUFULI AANZA KWA VITENDO KIGOGO
photogenic; LALA
MODEL AITWAE LALA NI MREMBO TOKA ATLANTA
No comments:
Post a Comment