Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Friday, February 4, 2011

MANJI NA MENGI KUTOANA MACHO...!!

  Mh.Manji akipata stata ya fegi huku akinakshinakshi akili yake kwa kupitia dokumenti
Mfanyabiashara nguli nchini, Yusuf Manji aliieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kuwa kashfa zilizotolewa na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Reginald Mengi kuwa yeye ni Fisadi Papa zimemvunjia heshima na kupoteza uaminifu wake mbele ya wabunge.
Aidha Hakimu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, anayesikiliza kesi hiyo inayovuta hisia za wengi nchini, Aloyce Katemana, alikubali kupokea vielelezo vya hati ya barua ya mwaliko wa Kamati ya Bunge zisizo halisi, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
     Fuso likishusha wingi wa magazeti ikiwa ni ushaidi mbele ya mahakama.
Manji alitoa nyaraka nane zisizo halisi (Original) ambazo ni mialiko ya shughuli za kiserikali ya ndani na nje ya nchi zilizodai kumtaka awe mgeni rasmi na kutoa hotuba mbalimbali za masuala ya kiuchumi.
Pia alitoa magazeti ya This Day na Kulikoni pamoja na DVD, ambavyo vyote vilipokelewa na mahakama kufanya jumla ya vielelezo vilivyopokelewa kufikia tisa.
Manji ambaye jana ilikuwa ni mara yake ya kwanza kupanda kizimbani hapo, alitoa maelezo hayo wakati akitoa ushahidi wake juu ya kesi hiyo.
Mfanyabiashara alikuwa akitoa ushahidi wake huku akiongozwa na jopo la mawakili maarufu wa kujitegemea nchini: Mabere Marando, Dk. Ringo Tenga, Richard Rweyongeza, Sam Mapande na Beatus Malima.
Manji ambaye anadai alipwe fidia ya sh moja kwa madai ya kukashfiwa na Mengi, aliwasili mahakamani na msafara wa magari mbalimbali likiwemo gari aina ya fuso lilobeba lundo la magazeti ambayo yanadaiwa kuchapisha habari iliyomnukuu Mengi akimkashifu ambayo yaliwasilishwa mahakamani hapo kama kielelezo.
Katika ushahidi wake, Manji alidai Aprili 23-27 mwaka 2009, Mengi kwa kutumia kituo cha televisheni cha ITV, alitoa madai kuwa Manji na wafanyabiashara wengine kuwa ni mafisadi papa, wanahamisha rasilimali za taifa kupeleka nje ya nchi na kwamba wameshiriki kikamilifu katika ufisadi wa ununuzi wa magari ya JWTZ, rada, mradi wa makaa ya mawe wa Mchuchuma, mifuko ya hifadhi ya jamii ya PSPF na NSSF, Dowans na Richmond.
Kwa mujibu wa Manji, Mengi alidai zabuni hizo walizipata kwa rushwa na fedha walizonazo zimetokana na ufisadi.
Mkanda wa kipindi hicho maalum, ulionyeshwa mahakamani hapo kama kielelezo cha ushahidi.

FFU WAVAMIA OFISI ZA GLOBAL PUBLSHER!

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Askari wa kutuliza ghasia (FFU) leo asubuhi badala ya kutuliza walikuwa chanzo cha fujo pale walipoingia kama wendawazimu katika ofisi za Kampuni ya Global Publishers na kuanza kupiga makofi na mabomu wafanyakazi.
Polisi hao walifika katika ofisi hizo ghafla huku wakiwa na bunduki na kuanza kufyatua mabomu ya machozi na baadaye polisi kadhaa waliingia ndani huku wakiwa wameshikilia bastola maalum ambapo kulikuwa na kikao cha kupitia magazeti kikiendelea, polisi mmoja  alitoka nje na mtumishi mmoja. Kifupi hali ilikuwa mbaya kutokana na kipigo cha polisi hao  kwa wafanyakazi wasiokuwa na hatia.
Kuona hali inazidi kuwa mbaya, Mhariri Mtendaji Manyota aliwasiliana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, (IGP) Saidi Mwema na kumueleza kila kitu kuhusiana na fujo za kikosi cha kutuliza ghasia ambapo kiongozi huyo alishtuka na kutoa pole huku akiahidi kushughulikia suala hilo.
PATA PICHA HALISI ZA TUKIO ZIMA!

Askari wa kutuliza ghasia (FFU) wakijaribu kumchukua mmoja wa wafanyakazi wa Global Publishers, Hassan Ally Daffa kwa madai kuwa ni mmoja wa wanafunzi walioandamana huku wafanyakazi wenzake wakimtetea.

No comments: