YAMEZUKA mapigano kati ya Waislam na Wakristo katika mji mdogo wa Mto wa Mbu wilayani Monduli, mkoani Arusha, na kusababisha wachungaji wawili kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Karatu kwa matibabu
Hadi tunakwenda mitamboni blogu hii ilikuwa na taarifa tofauti kuhusu chanzo cha vurugu hizo ambapo moja ilieleza kuwa chanzo cha vurugu hizo ni baadhi ya Waislamu kuwatuhumu wachungaji wawili waliotajwa kwa majina ya mchungaji Jakson na mwenzake Prospatus, kwamba wamekuwa wakiichambua vibaya Kurani tukufu hivyo kuidhalilisha dini ya Kiislam, hivyo wakaamua kuvamia mkutano wa Injili na kuwashambulia wachungaji hao pamoja na wasikilizaji wao.
Mbali na kuwajeruhi wachungaji hao, ilielezwa kuwa Waislam hao walivunja na kuliharibu kanisa la Anglikana la Mto wa Mbu.
Hata hivyo, taarifa nyingine kutoka Mto wa Mbu zilisema chanzo cha vurugu hizo ni mahubiri yaliyofanywa na mhubiri mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Utouh ambaye ilielezwa kuwa mahubiri yake aliyoyafanya kwa wiki nzima yalisababisha waumini wa Kiislam 20 wabadili dini na kuwa Wakiristo, hali ambayo ilidaiwa kuzusha chuki ya kidini katika eneo hilo.
“Walikwenda nyumbani kwa huyo mhubiri hawakumkuta, walivunja mlango wa nyumba yake na kutoa vitu vyote nje na kuvichoma moto.
“Walipotoka hapo walikwenda katika Mwalimu Anne Academy ambayo mwenye shule ni Mkiristo, hapo walivunja ofisi ya walimu ambao walikuwa madarasani na kuchukua simu za mikononi na kisha waliwapiga walimu na watoto,” zilieleza taarifa hizo kutoka kwa baadhi ya wananchi wa Mto wa Mbu waliodai kujua yaliyotokea.
Blog hii lilipowasiliana na kamanda wa polisi, OCD Maganga, alithibitisha kupata taarifa za tukio hilo na kwamba alikuwa njiani akielekea Mto wa Mbu kulifuatilia.
MODEL OF A WEEK
Oluchi,Nigerian super model:
Nigerian supermodel, Oluchi Onweagba-Orlandi looked stunning in the January 2011 Catalog for US Department Store, Nordstrom.
Oluchi rocked clothing from many of Nordstrom’s bestselling brands, including BCBG, Linea Pelle and DKNY.
MAPIGANO YA LIBYA YAIVA,SILAHA NZITO ZATUMIKA KUWAUA WALIBYA
Wanajeshi wanaomuunga mkono Kanali Muammar Gaddafi wametekeleza mashambulio katika miji iliyoko karibu na mji mkuu Tripoli, katika juhudi za kupanua maeneo wanayoyadhibiti.
Makabiliano makali yaliripotiwa magharibi mwa mji wa Zawiya ambapo walioshuhudia wamesema kuwa silaha nzito nzito zilitumika kuwashambulia waandamanaji ndani ya msikiti, na kuwaua takriban watu wasiopungua kumi.
Mashariki mwa mji kumetokea makabiliano makali kupigania udhibiti wa uwaja wa ndege ulioko karibu na mji wa Misurata.
Daktari mmoja ameiambia BBC kuwa hospitali yake imepokea majeruhi wapatoa 70.Mkaazi mmoja anasema wanajeshi watiifu kwa Kanali Gaddafi wamefikuzwa kutoka mji huo.
Huku hayo yakiarifiwa, rais Barack Obama wa Marekani ametoa wito kwa viongozi wa Uingereza, Ufaransa na Italia washauriane juu ya hatua za kuchukua kukabili mzozo wa Libya
Duru za awali kutoka Ikulu ya white house zilidokeza kuwa Obama anazingatia hatua kadhaa dhidi ya serikali ya Libya ikiwemo kuwekewa vikwazo.
PICHA ZA LEO:
Ben kinyaiya akiwa taabsani kwa mazoezi yanayoendelea leaders club.
Timu ya Bongo Movie Fc wameanza kujifua leo katika viwanja vya Leaders kwa ajili ya maandalizi makubwa dhidi ya Wapinzani wao Bongo Fleva Fc.Mchezo huo ambao ni maalumu kwa ajili ya kuchangia waathirika wa Mabomu ya Gongolamboto umeanza kuvuta hisia za watu na mashabiki wengi katika jiji la Dar es salaam.Kila timu inajitamba kivyake lakini sisi tunasema ushindi ni lazima siku hiyo ya jumamosi.Mashabiki mnaombwa kijitokeza kwa wingi ili kuchangia ndugu zetu wa GongolambotoWizara ya sayansi na Technolojia mmeona ubunifu wa hawa watoto
Mbunifu mashuhuri Tanzania Ali rehmtulah akiwa na vazi la kipekee mmmh...!!
uniquetz t0p 40 gorgious women 2011
1. Sofia Vergara
2. Natalie Portman
3. Amanda Seyfried
4. Katy Perry
5. Brooklyn Decker
6. Inez Sainz
7. Mila Kunis
8. Selita Ebanks
9. Minka Kelly
10. Bar Rafaeli
Nawashukuru sana watu wote waliokuwa wanafatilia top 40 yetu .am magese c u next tym.......bye bye!
No comments:
Post a Comment