Kundi la kwanza la wanafunzi hao lilijikusanya katika Viwanja vya Mnazi Mmoja majira ya mchana na kuanza maandamano hayo yaliyokuwa na lengo la kumfikishia ujumbe Rais Jakaya Kikwete wa kutoridhishwa na ongezeko hilo la nauli. Kundi jingine la wanafunzi lilianzia maandamano hayo katika Uwanja wa Karume.Wanafunzi wa shule za sekondari za jijini Dar es Salaam wakiwa na mabango karikaoo jana wakati wakiandamana kupinga ongezo la nauli za daladala, wakidai kwamba nauli mpya ni kubwa mno hawataimudu wakitaka wapunguziwe. Picha na Robert Ben-Baya Mwandishi wa habari hii alipofika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja aliwakuta wanafunzi hao wakijipanga kuanza maandamano hayo huku wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali. Baadhi ya mabango hayo yalisomeka: ‘Kama ni maji ya pilipili, hayawezi kuwa suluhisho la migomo.’
Baadhi ya wanafunzi walisema wameamua kupinga nauli hiyo mpya kwa maandamano ili kuishinikiza serikali iifute wakitaka kurejeshwa kwa ile ya zamani ya Sh100 ili kuwapunguzia mzigo wazazi wao kuwasomesha.
“Sisi wengine kwa siku tunapanda magari matatu hadi kufika shule na hapo bado hujala. Sasa kwa hali hii kweli tutasoma?" Alihoji mmoja wa wanafunzi hao.
Mwanafunzi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Habib Juma alisema nauli ya Sh150 kwa mwanafunzi ni kubwa mno kuimudu akisema kipato cha wazazi wengi ni duni na baadhi yao wanashindwa hata kutoa michango mbalimbali ya shule.
Hata hivyo, jitihada za wanafunzi hao kufikisha ujumbe wao Ikulu ziligonga mwamba baada ya kudhibitiwa na FFU muda mfupi tu baada ya kuingia barabarani.Askari hao waliokuwa na pikipiki walitanda barabarani na kuwatawanya wanafunzi hao na baadaye waliwashikilia wanafunzi wawili wa kiume baada ya wenzao kukimbia. Wanafunzi hao walipakiwa kwenye gari la polisi na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Msimbazi.
Nauli hizo mpya za daladala zilizotangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), wiki iliyopita zilianza kutumika rasmi jana.Ofisa Mfawidhi wa Sumatra katika Kanda ya Dar es Salaam, Conrad Shio alisema nauli hizo zimegawanywa katika makundi matatu kwamba wanafunzi watatozwa Sh150 kwa safari, kundi la pili ni njia zenye nauli moja ya Sh300 na la tatu ni la njia zenye nauli zaidi ya moja na kwamba nauli hizo zimeongezeka kwa Sh50 katika nauli za awali, katika kila safari moja.
Shio alitoa mfano akisema kwa njia ambayo abiria wake walikuwa wanatozwa nauli ya Sh250 kwa safari, sasa watatozwa Sh300.Alisema katika Kanda ya Mashariki nauli ya juu zaidi itakuwa Sh1,700 kwa safari kati ya Kigamboni na Pembamnazi, eneo ambalo awali nauli yake ilikuwa Sh1,300.
Sumatra imeongeza nauli hizo baada ya kupokea maombi ya wamiliki wa mabasi mwishoni mwa mwaka jana wakilalamikia kupanda kwa gharama za uendeshaji.
MARLAW NA BESTA KUFUNGA NDOA JUMAMOSI HII
Wasanii 2 ma-star wa Muziki wa Kizazi kipya toka TZ,Lawrence Malima aka Marlaw na Besta Rugeiyamu aka Besta,kesho Jumamosi ya tarehe 11 March 2011 wanatarajiwa kufunga pingu za maisha aka kuoana.
Marlaw na Besta walikua na uhusiano wa Chini ya Carpet na kwa sasa mambo yako hadharani,coz alhamisi iliyopita kulikua na Kitchen Party ya Besta na Jumamosi pia ya wiki iliyopita kulikua na Send Off ya Besta ambapo aliagwa rasmi na familia yake. NDOA NJEMA....KILA LA KHERI!
SIKU NA MATUKIO
Jamani kama nyinyi ni wakumbukaji wa bata za hapa mjini ,hapa ni wapi? WATU 700 WAFARIKI,1500 HAWAJULIKANI WALIPO, 800 WAJEHURIWA JAPAN KWA TETEMEKO KUBWA LA ARDHI(TSUNAMI)
Tetemeko kubwa la ardhi limepiga kaskazini-mashariki mwa Japan, na kuibua mawimbi ya tsunami ambayo yamesababisha hasara kubwa
Televisheni nchini Japan, imeonesha magari, meli na hata majengo makubwa yakizolewa na mawimbi makubwa ya maji ya bahari baada ya tetemeko lenye ukubwa wa 8.9 kupiga.
Tetemeko hilo pia limesababisha moto katika maeneo mengi ya Japan ikiwemo mji mkuu Tokyo, ambapo imearifiwa watu 15 wamekufa.
Limepiga kiasi cha kilometa 400 kutoka mji mkuu na mawimbi yakaingia umbali wa maili 20 ndani.
Wataalam wa matetemeko wamesema hili ni moja ya tetemeko kubwa kuipiga Japan kwa miaka mingi.
Wakati tetemeko lilipopiga, majengo mjini Tokyo yaliyumba. Mtu kutembea ilikuwa sawa na kuwemo ndani ya meli inayopigwa mawimbi baharini.
Watu walishuka chini kutoka katika ofisi zao na kusalia mitaani wakiwa wanatetemeka.
Moto mkubwa ulizuka katika eneo moja la mji na katika maeneo mengine, watu waliojeruhiwa walitolewa nje ya vituo.
Mara moja serikali ilitoa onyo la tsunami.
Katika mji mkuu Tokyo, usafiri wa umma umesimamishwa, lifti katika majengo mengi zimezimwa na maelfu ya watu wamekusanyika katika bustani za wazi na vituo vya treni.
Onyo la tsunami limetolewa pia katika maeneo yote ya bahari ya Pacific ikiwemo Philippines, Indonesia, Taiwan, Hawaii, na mwambao wa bahari ya Pacific nchini Urusi na kaskazini mwa Amerika Kusini.
Mawimbi makubwa yalipiga katika miji ya Miyagi na Fukushima, na kuharibu vibaya sehemu kubwa ya makazi ya watu eneo la pwani. Shirika la habari la Kyodo limesema mawimbi yaliyofikia urefu wa mita 10 na kupiga bandari ya Sendai huko Miyagi .
Televisheni nchini Japan, imeonesha magari, meli na hata majengo makubwa yakizolewa na mawimbi makubwa ya maji ya bahari baada ya tetemeko lenye ukubwa wa 8.9 kupiga.
Tetemeko hilo pia limesababisha moto katika maeneo mengi ya Japan ikiwemo mji mkuu Tokyo, ambapo imearifiwa watu 15 wamekufa.
Limepiga kiasi cha kilometa 400 kutoka mji mkuu na mawimbi yakaingia umbali wa maili 20 ndani.
Wataalam wa matetemeko wamesema hili ni moja ya tetemeko kubwa kuipiga Japan kwa miaka mingi.
Wakati tetemeko lilipopiga, majengo mjini Tokyo yaliyumba. Mtu kutembea ilikuwa sawa na kuwemo ndani ya meli inayopigwa mawimbi baharini.
Watu walishuka chini kutoka katika ofisi zao na kusalia mitaani wakiwa wanatetemeka.
Moto mkubwa ulizuka katika eneo moja la mji na katika maeneo mengine, watu waliojeruhiwa walitolewa nje ya vituo.
Mara moja serikali ilitoa onyo la tsunami.
Katika mji mkuu Tokyo, usafiri wa umma umesimamishwa, lifti katika majengo mengi zimezimwa na maelfu ya watu wamekusanyika katika bustani za wazi na vituo vya treni.
Onyo la tsunami limetolewa pia katika maeneo yote ya bahari ya Pacific ikiwemo Philippines, Indonesia, Taiwan, Hawaii, na mwambao wa bahari ya Pacific nchini Urusi na kaskazini mwa Amerika Kusini.
Mawimbi makubwa yalipiga katika miji ya Miyagi na Fukushima, na kuharibu vibaya sehemu kubwa ya makazi ya watu eneo la pwani. Shirika la habari la Kyodo limesema mawimbi yaliyofikia urefu wa mita 10 na kupiga bandari ya Sendai huko Miyagi .
QUEEN SUZY WA TWANGA PEPETA ARUDI FM ACADEMIA
Mnenguaji nyota katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini, mbaye alikuwa akiitumikia bendi ya The African Stars 'Twanga Pepeta' Susan Chubwa almaarufu kwa jina la ‘Queen Suzy’ kesho usiku anatarajiwa kutambulishwa rasmi katika bendi yake ya zamani FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma' , utambulisho huo utafanyika katika onyesho lao ambalo litakalofanyika katika ukumbi wa Kijiji Cha Makumbusho.Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam leo mchana , Queen Suzy amekiri kuwa, amerudi tena kuitumikia bendi ya FM Academia na kuanzia kesho ataonekana katika maonyesho yote ya bendi hiyo.
Waasi waukimbia mji wa Ras Lanuf
Waasi wa Libya wanakimbia bandari ya mafuta ya Ras Lanuf baada ya mashambulio yaliyofanywa na majeshi yanayomtii Kanali Muammar Gaddafi.
Ripoti zinasema waasi walikuwa wakielekea na magari upande wa mashariki baada ya kushambuliwa na makombora.
Televisheni ya taifa ya Libya ilisema majeshi yanayomwuunga mkono Kanali Gaddafi pia yamewaondosha waasi kwenye bandari ya mafuta ya Sidra, magharibi mwa Ras Lanuf.
Katika siku za hivi karibuni, majeshi ya Kanali Gaddafi yamejaribu kudhibiti maeneo ya mashariki yaliyoshikiliwa na waasi, pamoja na mji wa Zawiya, magharibi mwa Tripoli.
Huko Ras Lanuf, muasi mmoja aliliambia shirika la habari la AFP: " Tumeshindwa. Wanarusha makombora na sisi tunakimbia. Hii inamaanisha wanadhibiti Ras Lanuf"
Ndege za UN zapigwa marufuku Ivory Coast
Serikali yenye utata ya Rais Laurent Gbagbo imepiga marufuku ndege za majeshi ya usalama ya Umoja wa Mataifa na Ufaransa kupita kwenye anga ya nchi hiyo, au kutua Ivory Coast.
Tamko hilo limetolewa huku Alassane Ouattara, anayetambulika na Umoja wa Mataifa kama mshindi wa uchaguzi uliofanyika mwezi Novemba, alipokwenda kwenye mkutano nchini Ethiopia juu ya mgogoro huo.BBC imefahamishwa kuwa Umoja wa Afrika AU, unatarajia kutoa wito kwa Bw Ouattara kuongoza serikali ya umoja.
Bw Gbagbo amekataa kuhudhuria mkutano huo wa AU.
Mwandishi wa BBC Uduak Amimo aliyopo katika mkutano huo kwenye mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, alisema haijfahamika wazi iwapo mpango huo uliopendekezwa wa serikali ya umoja wa kitaifa utabakiza nafasi ya Bw Gbagbo, lakini bila shaka utahusisha baadhi ya wanaomtii kiongozi huyo.
Kundi la wakuu watano wa nchi za Afrika wamekuwa wakijaribu kutatua pingamizi la kisiasa huku kukitolewa onyo la nchi hiyo kurejea kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Uchaguzi wa mwaka jana uliochukua muda mrefu ulitakiwa kuunganisha upya nchi hiyo- ambayo ilikuwa moja ya nchi tajiri Afrika Magharibi- iliyogawanyika tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 2002.
Tume ya uchaguzi inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imesema Bw Ouattara alishinda uchaguzi wa Rais mwezi Novemba, lakini baraza la katiba lilibatilisha matokeo hayo, kwa madai ya kufanyika hila.
SHINDANO LA MISS UTALII TAIFA CHIPUNGAHELO DESH..DESH..NA FUNDI MITAMBO UKUMBINI
MKURUGENZI wa shindano la Taifa la Miss Utalii, Gideon Chipungahelo, amedaiwa kumtwanga fundi mitambo aliyekuwa akisimamia suala la taa katika ukumbi wa Hoteli lilipofanyika shindano hilo hivi karibuni mjini Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Chipungahelo, alimfuata na kuanza kumporomoshea magumi mazito fundi mitambo huyo baada ya umeme kuzimika ghafla ukumbini humo wakati shindano hilo likiendelea huku likiwa linarushwa live na moja ya Kituo cha Televisheni.
Baada ya kutokea tukio hilo, Chipungahelo aliyekuwa Mc wa shindano hilo huku 'akihozi' kuongoza kila idara iliyokuwa ikishughulika na shindano hilo, alishuka jukwaani huku likiwa limetawala giza totoro na kutimua mbio kuelekea katika chumba alichokuwapo jamaa huyo.
Ghafla mashabiki wa shindano hilo waliokuwa ukumbini humo pamoja na mapaparazi, walimsikia jamaa huyo akipiga kelele za kuomba msaada kwa kupokea kipigo kitakatifu kutoka kwa Chipungahelo, aliyekuwa akifanya hivyo huku akiwaka kwa sauti, “Unataka kuniharibia shughuli”. Alisikika akisema Chipungahelo.
Hata hivyo mashabiki wa shindano hilo walisikika wakilalama ukumbini humo kutokana na utaratibu wa Mkurugenzi huyo anavyoendesha shindano hilo, na kumtupia lawama lukuki kwa kupanga matokeo na kumpa ushindi mshiriki ambaye wao wanazani hakustahili kushinda.
Baadhi ya wazazi wa washiriki hao walisikika wakilalama ukumbini humo kuwa hawakubaliani na matokeo hayo kwa vile washindi wa tatu bora waliochaguliwa hawakukidhi vigezo na hawakua na mvuto mbele ya mashabiki ukumbini humo.
Shindano hilo liliwaboa watu zaidi pale lilipovunja rekodi ya kuchelewa kuanza, ambapo lilianza mida ya saa tano usiku na kumalizika saa kumi na mbili kasoro za alfajiri siku iliyofuata.
Akizungumza na Sufianimafoto Mkurugenzi wa Shindano hilo, Gideon Chipungahelo, alikili kutokea kwa mshike mshike huo na kusema kuwa, alilazimika kumtwanga magumi fundi huyo baada ya kugundua kuwa alikuwa amehujumiwa kutokana na shindano hilo kuwa likirushwa live.
“Unajua muda mwingine inabidi uwe Baunsa tu kwani niligundua mipango ya wazi kabisa ya kuniujumu na kuharibu shindano langu tangu mapema na ndiyo maana baada tu ya kutokea tukio hilo la kukatika kwa umeme nilimwendea moja kwa moja aliyekuwa akihusika na idara hiyo, ambaye hakuwa na majibu ya kuniridhisha,
Na ndiyo hasa sababu iliyonifanya kuanza kumtwanga magumi potelea mbali kama nilionekana tofauti kwa muda ule kwani tayari nilishapandwa na ghadhabu kutokana na kuharibikiwa tena mbele ya mashabiki waliokuwapo ukumbini na watu waliokuwa katika Luninga zao majumbani wakifuatilia shindano hilo” alisema Chipungahelo.
Mshindi wa kwanza wa shindano la Taifa la Miss Utalii 2010, Adelqueen Njozi (wapili kulia) akiwa na washindi wenzake, mshindi wa pili Happywhitney Andrew kutoka mkoa wa Pwani, (wapili kushoto), mshindi wa tatu Mariam Rabii kutoka Mkoa wa Ruvuma (kulia) na Mshindi wa Kipaji, Kokuletage Mushumbusi (kushoto) wakati walipofika kwenye Ofisi za Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo mchana kutambulishwa baada ya shindano hilo kumalizika mwishoni mwa wiki iliyopita Bagamoyo. Warembo hao wakiwa jukwaani wakati wa shindano hilo kabla ya kukatika kwa umeme na kuzua mtafaruku
Na sufian maphoto.mwandishi wa hii habari.sio mimi
"""""""""""""""""""
"""""""""""""""""""
salam,
Natumai ya kua utakua mzima wa njema afya mimi pia niko salama kabisa, kwanza hongera sana kwa kazi zako za blog ikiwa ni pamoja na kutuletea habari mbali mbali za nchini kwetu, Duniani burudani na michezo big na Mwenyezi Mungu akubariki uendelee mbele zaidi wewe pamoja na timu yako nzima ya matukio.
Kwa niaba ya timu nzima ya Mbeya yetu blog,tulikua tunaomba msaada wako wa kututambulishia libeneke letu jipya la Mbeya yetu, Tunatanguliza shukrani zetu. Asante sana.
JINA LA BLOG: MBEYA YETU
Tunapenda kulitambulisha wadau wote libeneke jipya la Mbeya Yetu ambapo nia na malengo ni kuwaletea habari mbali mbali kutoka Jijini Mbeya, Tanzania na Duniani kwa Ujumla ikiwa unatukio la aina lolote usisite kututumia kupitia mbeyayetu@yahoo.com . karibuni nyote na asanteni kwa kututembelea.
Toccara Jones from Dayton, Ohio, is an American fashion model, occasional actress and television personality. Jones was a contestant on the third season of the UPN series America's Next Top Model, where she finished in seventh place. She was the eighth contestant eliminated on the third cycle of America's Next Top Model, where she won "Covergirl of the Week" five times. She was recently voted as one of the most memorable contestants by AOL Entertainment. Since ANTM, Jones signed with Wilhelmina Models as a plus-size model. She has been on the covers of Be, The Next Level Magazine (November 2005), Black Men magazine, Black Hair magazine, Braids magazine, and King magazine (February/March 2006, March/April 2006, and April 2008). She appeared in the December 2008 issue of Ebony magazine.
plus size model
No comments:
Post a Comment