Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Saturday, March 19, 2011

BUNGE LIJALO ITAKUWA VITUKO TUPU!

                         Anna Makinda - spika wa bunge la Tz
  Ile kauli ya spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania mh. Anna makinda  kusema kuwa zomea zomea na vijembe ruksa  bungeni  huenda ikalifanya bunge hilo kuwa  sehemu  ya mzaha na kejeri zisizo na manufaa kwa wapiga kura .
  Bunge ni chombo tukufu kwanini isiwe sehemu ya kudumisha upendo kati ya chama tawala na vyama vya upinzani  kwa staili ya kuzomeana naamini baadhi ya wabunge hawatoridhika nakitendo hiko kinahofiwa kuzua  chuki sizizo na tija kwa taifa
  Wito umetolewa kwa spika wa bunge uachana na utamaduni wa kuiga wa mabunge y a nchi za maharibi ikiwemo kuzomeana,marumbano yasiyo na msingi na kejeri zinazoelekeza hisia za kutofautiana kihisia,hatari  ni kuwa ikiruhusiwa sana vitendo hivyo ipo siku wabunge watashikikana mshati kama si kurushiana viti bungeni kama ilivyowahi kutokea nchini Kenya.


100ml zayayuka simba yalambwa 3-1 na tp mazembe


Kikosi cha simba kilichoenda lubumbashi na kukimbia poli la wazaire kwa kubugizwa 3-1

 

Chelsea yaichapa Man City

Chelsea imejikita katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ya England, baada ya kuichapa Manchester City kwa mabao 2-0.
Luiz
David Luiz aliandika bao la kwanza

Wakicheza bila Carlos Tevez, City hawakuonesha cheche zozote, ingawa Yaya Toure aliachia mkwaju mmoja uliookolewa na Peter Cech.
Wakisaidiwa na chenga za Salomon Kalou, Chelsea walifanya mashambulizi baada ya mapumziko, ba beki David Luiz kufunga kwa kichwa, zikiwa zimesalia dakika 12.
Bao la pili lilifungwa na Ramires, alipowapiga chenga mabeki wa City katika dakika za majeruhi na kupachika bao maridadi.
Suarez
Luis Suarez

Katika mchezo mwingine, penati yenye utata na uchezaji maridadi wa Luis Suarez umeipa ushindi Liverpool dhidi ya Sunderland.
Sunderland ilifungwa bao la kwanza baada ya mkwaju wa penati uliopigwa na Dirk Kuyt, baada ya John Mensah kumfanyia madhambi Jay Spearing.
Refa Kevin Friend awali alisema upigwe mpira wa adhabu, kabla ya kubadili mawazo na kuufanya mkwaju wa penati, baada ya kumsikiliza mshika kibendera.
Suarez alipachika bao la pili baada ya mapumziko, baada ya kukatiza katika upenyo mdogo.

Jeshi la Ufaransa latanda Libya

Ndege za kijeshi za Ufaransa zinazuia majeshi yanayomtii kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi kushambulia mji unaodhibitiwa na waasi wa Benghazi, amesema rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy.
Ndege
Ndege ya Ufaransa

Inaaminika kuwa hii ndio hatua ya kwanza ya kuingilia kati mzozo huo tangu Umoja wa Mataifa kupiga kura siku ya Alhamisi, kufunga anga ya Libya.
Viongozi wa nchi za Magharibi na za Kiarabu, wamekuwa wakikutana mjini Paris, Ufaransa kujadili jinsi ya kumkabili Kanali Gaddafi.
"Ndege zetu zitazuia ukandamizaji wowote," amesema Bw Sarkozy.
Saa kadhaa mapema, majeshi yanayomuunga mkono Kanali Gaddafi yalifanya mashambulio katika ngome ya waasi mjini Benghazi, ameshuhudia mwandishi mmoja wa BBC.
ndege
Ndege ya kivita ya Ufaransa

Hata hivyo seikali ya Libya imekanusha kufanya mashambulio.
Ndege za kijeshi za Ufaransa pia zimeruka katika "anga yote ya Libya" katika kufanya doria, zimesema taarifa za jeshi la Ufaransa.
Ndege za kijeshi za Ufaransa ziliondoka katika kituo cha kijeshi cha Saint-Dizier, mashariki mwa Ufaransa, zimesema taarifa zilizokaririwa na shirika la habari la Agence France-Presse.
Ndege hizo hazikupata tatizo lolote katika saa kadhaa za mwanzo za hatua hiyo, zimesema taarifa hizo, na kuongeza ndege hizo zitaendelea kupaa kwa saa kadhaa zaidi.
Marekani itatumia "uwezo wake wa kipekee" kuimarisha kufungwa kwa anga, amesema waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Hilary Clinton, na kuonya kuwa kuchelewa zaidi kutahatarisha wananchi zaidi. Hata hivyo Bi Clinton amesisitiza kuwa Marekani haitapeleka wanajeshi wa ardhini nchini Libya.


Makaazi ya Kanali Gaddafi yashambuliwa

Ndege zake za kijeshi, zimeshambulia makaazi ya Kanali Gaddafi mjini Tripoli na kusababisha uharibifu mkubwa kwenye jengo moja.
Viongozi wa muugano wa majeshi hayo wanasema jengo lililoharibiwa lilikuwa linatumika kuamrisha majeshi ya Libya yanayopigana na waasi.
Waandishi wa habari wametembezwa kwenye eneo hilo lakini hakuna taarifa ikiwa maafa yalitokea baada ya shambulizi hilo.
Naibu mkuu wa jeshi la wanamaji wa marekani Bill Gortney anasema mashubulizi hayo hayaja mlenga kanali Gaddafi.
vifaru vya serikali vinateketea

Televisheni ya Libya imeonesha maiti na magari ya kijeshi yaliyoteketea kwenye barabara ya kuelekea mji wa Benghazi, shina la wapinzani wa serikali
Msemaji wa serikali ameeleza kuwa watu 64 wameuwawa katika mashambulio yaliyofanywa na mataifa ya magharibi, lakini hakuna njia ya kuthibitisha taarifa hiyo.
Awali afisa mkuu wa jeshi la Marekani, , Mike Mullen, alisema ndege kutoka Qatar zinapelekwa huko, kuwa tayari kushiriki katika operesheni dhidi ya Libya, na nchi nyengine piya zimetoa ahadi kusaidia.
Adimeri Mullen alieleza kuwa agizo la Umoja wa Mataifa, la kuzuwia ndege za serikali kuruka katika anga ya Libya, sasa limetekelezwa, na majeshi ya Kanali Gaddafi, katika mji wa Benghazi, unaodhibitiwa na wapinzani, sasa hayawezi kusonga mbele.
Alisema hakuona taarifa, kuwa raia wameuwawa.
mpinzani na bunduki yake karibu na Benghazi
mpinzani na bunduki yake karibu na Benghazi

Urusi imetoa wito kwa Uingereza, Ufaransa na Marekani, ziache kushambulia maeneo yasiyokuwa ya kijeshi, na kwamba raia wameshambuliwa.
Mkuu wa Jumuiya ya Kiarabu, Amr Moussa, amesema mashambulio yamekwenda mbali, kushinda lile lengo la kulinda tu anga ya Libya, ambavyo ndivo jumuiya yake ilivotaka.

Mapigano yameenea katika maeneo mapya nchini Cote d'Ivoire

Marekani imewaonya raia wake wasisafiri kwenda Cote d'Ivoire. Matangazo ya vyombo vya habari vya kimataifa yamefungwa Cote d'Ivoire huku rais Gbgabo akivilaumu kwa kuitingisha nchi

Milipuko imesikika katika kitongoji kimoja kusini mwa mji mkuu wa Cote d'Ivoire, Abidjan usiku kucha na hapo jana, huku mapigano kati ya waasi wanaotaka kumuondoa madarakani kiongozi anayeng'ang'ania madaraka nchini humo Laurent Gbagbo na vikosi vya usalama, kuenea katika maeneo mapya mjini humo. Wakaazi wa kitongoji cha Koumassi wamesema milio ya risasi ilisita jana jioni na watu kadhaa walitoka nje ya nyumba zao, lakini watu wapatao wawili waliuwawa katika ufyatulianaji wa risasi.
Mbali na mapigano kadhaa katika kitongoji cha Adjame, kilicho karibu na eneo la katikati la biashara mjini Abidjan, mapigano mengi yamekuwa yakitokea katika kitongoji cha Abobo kaskazini mwa mji huo, ambacho ni ngome ya kiongozi wa upinzani Alassane Ouattara, anayetambuliwa na jumuiya ya kimataifa kama mshindi halali wa uchaguzi wa urais uliofanyika Novemba 28 mwaka jana.
Serikali ya Gbagbo imeanza kulipa mishahara wiki hii na imeyalenga matawi ya benki ya Societe Generale na BNP Paribas ili kuyataifisha, kama sehemu ya juhudi zake za kuusaidia uchumi usiporomoke. Benki ya Societe Generale imelaani vikali kuchukuliwa kwa tawi lake nchini humo pamoja na kutishwa kwa wafanyakazi wake.
Sambamba na hayo Marekani imewaonya raia wake dhidi ya kuitembelea Cote d'Ivoire. Wizara ya mambo ya ndani ya Marekani imewataka Wamarekani wajiepusha kwenda nchini humo hadi watakaposhauriwa kufanya hivyo. Imesema huku shinikizo dhidi ya Gbgabo likizidi, ukatili dhidi ya raia wa nchi za magharibi, wakiwemo Wamarekani, unaonekana kuongezeka. Inatarajia uchumi wa Cote d'Ivoire kuanguka, uhaba mkubwa wa nishati, chakula na mahitaji mengine, pamoja na mfumuko wa bei, mambo ambayo huenda yakasababisha hali ngumu kimaisha na kuzuka machafuko na uhalifu.
Wakati huo huo waasi kaskazini mwa Cote d'Ivoire wanasema mamilioni ya wakaazi wa eneo hilo wamekatiwa maji na umeme kwa kumuunga mkono Ouattara. Taarifa ya kampuni ya kitaifa ya umeme inasema wanaume waliokuwa na silaha walikatiza huduma za umeme Jumatatu wiki hii.
Kampuni hiyo imekuwa chini ya usimamizi wa rais Gbgabo aliyeitaifisha baada ya Umoja wa Mataifa kumtambua Ouattara kama mshindi wa uchaguzi wa Novemba mwaka jana.
Kwa upande mwingine matangazo ya radio ya BBC na Radio France International, RFI, hayakusika hewani hapo jana. Shirika la utangazaji la BBC limesema kwenye tovuti yake kuwa Laurent Gbagbo amekanusha kuchukua hatua dhidi ya vituo hivyo na halifahamu kwa nini matangazo yake yalisita. Gbagbo anavilaumu vyombo vya habari vya kimataifa kwa kuiyumbisha Cote d'Ivoire.
Kwa upande mwingine, Umoja wa Mataifa umekiri ulifanya makosa kuishutumu Belarus kwa kuipelekea Cote d'Ivoire helikopta za kivita. Kiongozi wa tume ya kulinda amani ya umoja huo, Alain Le Roy, amewaambia waandishi wa habari jana mjini New York Marekani kuwa aliomba radhi kwa serikali ya Belarus kwa niaba ya Umoja wa Mataifa kwa ripoti hiyo ambayo haikuwa sahihi.
Jumapili wiki hii ofisi ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon iliripoti kuwa helikopta moja ilikuwa imewasili Abidjan na kwamba helikopta zaidi zilikuwa zimepangwa kuwasili Jumatatu. Le Roy alisema taarifa hiyo ilitolewa na jopo huru la wataalamu linalosimamia vikwazo dhidi ya Cote d'Ivoire.

STARS v JAMHURI YA AFRIKA YA KATI KUKIPUTA LEO



Mechi ya mchujo ya Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) kati ya Taifa Stars na Jamhuri ya Afrika ya Kati itachezwa Machi 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo viingilio ni kama ifuatavyo; Viti vya Kijani na Bluu sh. 3,000, Viti vya Rangi

Tiketi zitaanza kuuzwa Machi 24 mwaka huu saa 2 asubuhi katika vituo vifuatavyo; Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Big Bon Msimbazi (Kariakoo), Mgahawa wa Steers (Mtaa wa Samora/Ohio), Kituo cha Mafuta OilCom (Ubungo), Uwanja wa Uhuru, Kituo cha Mafuta Kobil (Buguruni) na Kituo Kidogo cha Polisi Tandika Mwisho.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litatoa asilimia moja ya mapato yatakayopatikana katika mechi hiyo kusaidia waathirika wa maafa ya mabomu ya Gongo la Mboto.

Chelsea na Man U kukutana kombe la Ulaya

Droo iliyofanywa muda mfupi uliopita imeziweka Chelsea na Manchester United njia panda ambapo vilabu hivyo vitachuana kutafuta nafasi ya kushiriki nusu fainali.
Duru ya kwanza ya mpambano huo utafanyika kwenye uwanja wa Stamford bridge na ya pili kwenye uwanja wa Old Trafford ambapo Manchester United itaridhia kulipiza kisasi endapo mambo yatakwenda kinyume na matarajio yao katika pambano la kwanza.
Huu ni mfano wa marudio ya fainali ya mwaka 2008 Manchester United ilipoichapa Chelsea kupitia mikwaju ya penati mjini Moscow.
Ferguson
Ancelloti
Chelsea haijawahi kushinda Kombe la Ligi ya mabingwa na klabu hiyo inajitahidi kufanya vyema katika michuano hiyo ikiwa hali yake kwenye msimamo wa Ligi ya Premiership ni mbaya kiasi kuhitaji ushindi barani Ulaya ili msimu ujao isikose kushiriki michuano ya barani Ulaya.
Droo hiyo pia imeweka uwezekano wa mahasimu wa Ligi ya Uhispania kukutana kwenye hatua itakayofuata robo fainali. Barcelona itapambana na Shaktar Donetsk huku Real Madrid itachuana na Tottenham hotspurs.
Tottenham ambayo imekuwa kivutio cha mashindano haya kwa kuvibwaga vilabu vyenye uzoefu zaidi katika mashindano haya inaingia hatua ya robo fainali kwa nguvu kuwa Real Madrid haijawahi kushinda mbele ya klabu yoyote kutoka England.
Pamoja na hilo Real haijavuka hatua ya robo tangu mwaka 2002. Lakini safari hii ina kocha anayefahamu soka ya England, Jose Mourinho aliyeondoa rekodi ya vilabu vya Ufaransa kuiondoa Real Madrid katika mashindano haya kwa kipindi kirefu.
Endapo vilabu vya Uhispania vitavuka hatua hii basi vitapambana mara nne katika kipindi cha majuma matatu.
Ancelloti
Real imepangiwa kukutana na Barcelona katika mchuano wa La Liga tarehe 17 kisha fainali ya Kombe la Mfalme tarehe 20 Aprili mbali na nusu fainali hii ya Ligi ya mabingwa itakayobidi vilabu kucheza nyumbani na ugenini kati ya tarehe 5 na 6 Aprili na mechi za marudiano tarehe 12 au 13 mwezi huo huo.

Bingwa mtetezi wa Kombe hili Inter Milan atakwaruzana na Schalke 04, akitazamiwa kuvuka bila matatizo kufuatia jinsi alivyorahisisha safari yake kwa kuichapa Bayern Munich.
Kikamilifu hivi ndviyo ratiba ilivyo.

Robo fainali (Aprili 5/6 na Aprili 12/13)
Real Madrid (UHISPANIA) v Tottenham Hotspur (ENG)
Barcelona (UHISPANIA) v Shakhtar Donetsk (UKR)
Chelsea (ENG) v Manchester United (ENG)
Inter Milan (ITA) v Schalke 04 (GER)


The CFDA 2011 Nominees

MARC JACOBS will take home the CFDA's prestigious Geoffrey Beene Lifetime Achievement prize on June 6th at the 2011 CFDA Awards, it was announced in New York last night.

Jacobs is also in the running for the Womenswear Designer of the Year Award - the fourth time he has been nominated. He is up against Alexander Wang, Jack McCollough and Lazaro Hernandez of Proenza Schouler. The Menswear Designer of the Year accolade will be fought over by Michael Bastian, Patrik Ervell and Simon Spurr.

According to WWD, Lady Gaga will be presented with the Fashion Icon Award, while Phoebe Philo will be given the International Award for her work at Celine.

Here is the full list of nominees and winners:
International Designer of the Year
Celine creative director Phoebe Philo
Geoffrey Beene Lifetime Achievement Award
Marc Jacobs
Fashion Icon of the Year
Lady Gaga
Womenswear Designer of the Year
The nominees:  Alexander Wang, Marc Jacobs, Jack McCollough and Lazaro Hernandez of Proenza Schouler
Menswear Designer of the Year
The nominees:
Michael Bastian, Patrik Ervell and Simon Spurr
Accessory Designer of the Year
The nominees:
Reed Krakoff, Alexander Wang and McCollough and Hernandez of Proenza Schouler
Swarovski Award for Womenswear
The nominees:
 Joseph Altuzarra, Ashley and Mary-Kate Olsen and Prabal Gurung
Swarovski Award for Menswear
The nominees:
Alexander Wang, Phillip Lim and Robert Geller
Swarovski Award for Accessory Design
The nominees:
Alejandro Ingelmo, Eddie Borgo, Jason Wu and Pamela Love


WIZ-KHALIFA: BLACK YELLOW IMEMTOA KINYAMA!

Some new, unreleased Khalifa who just recently inked a deal with Atlantic (congrats to Wiz).

No comments: