Happy Birthday to theUNIQUEENTERTZ.BLOGSPOT.COM
TUNAYO FURAHA KUWAJULISHA WASOMAJI WA BLOGU HII KUWA APRIL1,2010 TUNATIMIZA MWAKA MMOJA TOKA TUWE HEWANI,TUTUMIE SALAMU ZA BIRTHDAY TUTAZIWEKA HEWANI.kupitia uniqueentertz@yahoo.com, facebook: magese unique (am nothing without my funs)
RAIS JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA WIZARA YA MAJI
Gaddafi ashambulia miji muhimu ya waasi
Milio mingi ya milipuko ilisikika usiku kwenye mji mkuu wa Tripoli.
Katika mji unaoshikiliwa na waasi Misrata, mashariki mwa Tripoli, vifaru vya serikali vimekuwa vikishambulia eneo karibu na hospitali.
Kumekuwa pia na ripoti juu ya mapigano makali baina ya waasi na majeshi yanayomwuunga mkono Gaddafi mjini Ajdabiya.
Wakazi waliokimbia mji huo wameelezea kuwepo kwa makombora, milio ya risasi na nyumba kuwashwa moto.
Mashambulio ya anga
Kulingana na vyanzo vya jeshi vya Libya na vyombo vya habari vimesema, kuna ripoti za kuwepo mashambulio ya anga yaliyofanywa na nchi za magharibi kwenye mji wa Tajura.Na jeshi la Ufaransa limesema mashambulio ya anga yaliyofanywa na Ufaransa yamelenga kituo cha anga cha Libya ndani ya nchi hiyo nyakati za usiku.
Siku ya Alhamis, ndege za kijeshi za nchi za magharibi zimeripotiwa kushambulia mji wa Sebha kusini mwa Libya, kulingana na wakazi na taarifa kutoka vyombo vya habari.
Sebha, uliopo kilomita 750 kusini mwa Tripoli, ni eneo lililodhibitiwa vilivyo na ni kitovu cha kijeshi cha Kanali Gaddafi.
Pia kumeripotiwa kuwepo kwa mlipuko nyakati za usiku kwenye kituo cha kijeshi eneo la Tajura mashariki mwa Tripoli.
Hivi ndivyo kizazi cha wasichana wa siku hizi wanavyo vaa na kuweka mambo yao ya falagha hadharani, zamani ilikuwa ni nandra kumuona mwananke akiwa amevaa shanga "chachandu" nje namna hii. Na vitu hivi hupaswa kuvaliwa kwa heshima. Je hii ndo kwenda na fasheni au tunawafundisha nini watoto wetu? . Picha hii imepigwa jijini Dar es Salaam katika daladala msichana huyu akiteremka kituoni.
Polisi wa Uganda rawamani kwa utesaji raia
Kulingana na ripoti iliyotolewa na shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch HRW, kitengo maalum cha polisi cha Uganda kimefanya utesaji, kutumia nguvu kupita kiasi na mauaji holela.
Ripoti hiyo imesema maafisa wa kikosi maalum cha polisi huwapiga watu mara kwa mara na vifaa kama marungu, chupa na vyuma.Imesema katika matukio mengine walikuwa wakiwaingizia pini chini ya kucha za washukiwa.
Msemaji wa polisi wa Uganda alisema kumekuwa na ripoti za utesaji, lakini idadi yao imepungua.
Ripoti hiyo yenye kurasa 59 imetolewa kutokana na ushahidi wa zaidi ya watu 100 na waliokuwa washukiwa, familia zao, na waliokuwa kwenye kikosi cha polisi pamoja na ambao bado wapo kwenye nafasi hizo.
R.I.P MUIGIZAJI LIZ TAYLOR
Actress maarufu wa filamu duniani,Elizabeth Rosemond Taylor aka Liz Taylor amefariki dunia Jumatano ya tarehe 23 March,2011 akiwa na miaka 79,baada ya kulazwa kwa muda wa wiki 6 kwenye hospitali ya Cedars-Sinai Medical Center jijini Los Angeles-Marekani
Liz Taylor alizaliwa London tarehe 27 February 1932,alianza kuugua ugonjwa wa moyo tangu mwaka 2004 na enzi za uhai wake aliwahi ku-act movie zaidi ya 50 na kuwahi kuolewa zaidi ya mara 8 na waume tofauti,na mpaka anafariki ameacha watoto 4,wajukuu 10 na vitukuu 4
No comments:
Post a Comment