Watu watatu wameuwawa baada ya polisi kuwafyatulia risasi waandamanaji Bahrain.
Jeshi nalo limetangaza kuwekwa kwa amri ya kutotoka nje katika maeneo kadhaa ya mji mkuu Manama.
Amri hiyo itatekelezwa kuanzia saa kumi jioni hadi saa kumi alfajiri.
Wakati huohuo, harakati za kijeshi zinaendelea ili kudhibiti eneo la Pearl kutoka kwa waandamanaji waliopiga kambi hapo kwa majumaa kadhaa.
Vitoa machozi vimerushwa na kumekuwa na ripoti za milio ya risasi katika maeneo ya mji huo.
Kiongozi wa upinzani ameiambia BBC kuwa kumekuwa na mamia ya majeruhi na vifo vya watu watano.
Mapema madaktari waliiambia BBC kwamba vikosi vya kijeshi vilikuwa vikiwazuia kutibu watu waliokuwa wamejeruhiwa.
JESHI LA JAN PAULSEN ALITANGAZA
Kocha wa timu ya STARS JAN PAULSEN wakati akitangaza kikosi cha Taifa kitakachocheza na JAMHURI YA KATI
GOALKEEPERS
Shaban Kado, Juma Kaseja, Shaaban Dihile
DEFENDERS:
Shadrack Nsajigwa, Aggrey Morris, Nadir Haroub 'Cannavaro', Stephano Mwasika, Haruna Shamte, Juma Nyoso na Idrissa Rajab.
MIDFIELDERS:
Nurdin Bakari, Shabani Nditi, Jabir Aziz, Henry Joseph, Abdi Kasim na Mwinyi Kazimoto
ATTACKERS:
Dan Mrwanada, Nizar Khalfan, Mrisho Ngasa, Mohamed Banka, Athuman Machupa, John Bocco na Mbwana Samata.
Mtanzania 'awekwa kama mtumwa Uingereza'
Aliyekuwa mkurugenzi wa hospitali ameamuriwa kulipa paundi 25,000 kwa mwanammke mmoja wa Kiafrika ambaye amemweka kama mtumwa mjini London.
Mkurugenzi huyo alimweka kifungoni raia mmoja wa Tanzania kama mtumwa kwa miaka minne.
Wazee wa baraza walisikia jinsi Mwanahamisi Mruke alivyosafirishwa kwa ndege mwezi Oktoba 2006 na kulazimishwa kufanya kazi saa kumi na nane kila siku kwa Bi Saeeda Khan ambaye ana umri wa miaka 68.
Mahakama ya Southcrown ilisikiliza namna ambavyo Bi Mruke aliye na umri wa miaka 47 alivyonyimwa haki ya kuwa na hati yake ya kusafiria na uhuru wake, na jinsi alivyohimili madhila aliyopata ili kumsomesha binti yake Afrika.
Khan alishtakiwa kwa biashara haramu ya kusafirisha mtu Uingereza na kumfanyisha kazi bila ujira wowote.
Bi Mruke alisema "hatomsamehe" aliyemweka kifungoni.
"Nilijihisi kama mjinga, nilifanywa kuwa mtumwa," Bi Mruke alisema.
Baada ya kumleta Uingereza kutoka Tanzania, Khan kutoka Harrow, kaskazini magharibi mwa London, mwanzo alimpa paundi 10 kila mwezi na kumfanyisha kazi mchana kutwa kila alipohitajika.
Hata hivyo baada ya mwaka mmoja akaacha kumlipa.
"Hata pesa nilizokuwa nimeahidiwa kulipwa sikupewa. Na nahisi vibaya kuhusu hili" Bi Mruke alisema.
"Nilikuwa nikitaraji kuwa nitalipwa mshahara na kuyaboresha maisha yangu. Lakini matumaini yangu yote yalipotea na nguvu zangu zilididimia na nikaanza kuumwa.
Hatimaye ligi Misri kuanza Aprili 15
Ligi ya soka nchini Misri itaanza tena tarehe15 mwezi wa Aprili, baada ya kusimama kwa muda wa miezi mitatu kutokana na harakati za kimapinduzi zilizosababisha kuondoka madarakani aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Hosni Mubarak.
Chama cha soka cha Misri, kimesema ligi hiyo iliyoanza mwezi wa Agosti mwaka jana, sasa itamalizika tarehe 10 mwezi wa Julai.
Ligi ilisimamishwa mwishoni mwa mwezi wa Januari, kwa sababu ya maandano na ghasia mjini Cairo na miji mingine.
Taarifa hiyo imepokelewa kwa furaha na vilabu, ambavyo mapato yake yalikuwa yamekauka kwa kukosekana kwa ligi hiyo.
"Hili ni jambo tulilokuwa tukilisubiri kwa hamu kubwa vilabu vyote", mjumbe wa bodi ya klabu ya Al Ahly Khaled Mortagey ameiambia BBC.
"Mapato yote yalisimama kwa hiyo sasa tutaweza kuishi."
Kulikuwa na wakati watu walikuwa na wasiwasi mkubwa miongoni mwa vilabu kwamba ligi hiyo msimu huu isingechezwa tena.
Kwa mujibu wa Mortagey, wacheza soka wa nchi hiyo pia wamefurahishwa kufahamu ligi yao inarudi tena.
Ligi hiyo ilisimama mwezi wa Januari ikiwa imefikia nusu baada ya wimbi la harakati za kimapinduzi kuikumba Misri.
Vigogo wa Cairo, Zamalek, ambao wanapigania kuutwaa ubingwa wa ligi kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004, ndio wanaongoza wakiwa na pointi 32, wakiwa mbele kwa pointi tatu dhidi ya Ismaily, baada ya kucheza michezo 15.
Mahasimu wa Zamalek, Ahly, wanaowania nao kushinda ligi kwa mwaka wa saba mfululizo, wanashikilia nafasi ya nne wakiwa na pointi 26.
No comments:
Post a Comment