PROX WAR au Proxy Warfare ni vita inayopiganwa kwa kupitia sehemu
nyingine. Katika vita 'ya kawaida' mapigano huwa kati ya nchi na
nchi.Kwa mfano, Vita ya Kagera ilkuwa kati ya Tanzania na Uganda, na
mapambano yalitokea katika nch zote mbili.
Katika
proxy war hali ni tofauti. Nchi A inaweza kupigana vita na nchi B
katika nchi C.Yaani kwa ufasaha zaidi, kwa mfano, kuna mapambano katika
nchi C kati ya jeshi la nchi hiyo na waasi, kisha nchi A inapeleka
askari wake kuilisaidia jeshi la serikali la nchi C, na nchi B inapeleka
askari wake (au inasaidia kwa siri) kusaidia waasi wanaopigana na
serikali ya nchi C.
Naomba ieleweke kuwa mie
sio nabii wa waangamizi, kwa kimombo 'prophet of doom.' Ninachoongelea
hapa kinatokana tu na hali halisi ilivyo kwenye mapigano yanayoendelea
nchi DRC kati ya jeshi la Serikali ya nchi hiyo na kikundi cha waasi cha
M23.
Nchi yetu imetoa wanajeshi kadhaa
kushirikiana na Malawi na Afrika Kusini kuunda kikosi cha kulinda amani
nchini DRC. Lakini kuna taarifa kuwa waasi wa M23 wanapewa sapoti na
Rwanda (kama ni kweli au la,mie sina hakika...lakini lisemwalo
lipo...kwanini Rwanda ituhumiwe na si Kenya au Msumbiji?)
Sasa
tukiangalia hali ya uhusinao kati ya Tanzania na Rwanda katika siku za
hivi karibuni, na tukijikumbusha kauli ya Rais Paul Kagame kuwa
"atamsbiri (Rais Jakaya) Kikwete mahala mwafaka kisha amtandike" kuna
uwezekano "mahala hapo mwafaka" kuwa ni DRC.
Kwanini
ninasema hivyo? Uwezekano wa Rwanda kuivamia Tanzania au Tanzania
kuivamia Rwanda ni mdogo sana,kutokana na sababu mbalimbali. Lakini nchi
hizo mbili zinaweza 'kupigana vita kirahisi' kupitia mapigano
yanayoendelea kati ya Jeshi la DRC linalosaidiwa na 'Kikosi cha
Kimataifa' (kinachojumuisha Jeshi la Tanzania) na waasi wa M23
(wanaodaiwa kusaidiwa na Rwanda.)
Vyovyote
itakavyokuwa, vita ni kitu kibaya, natunapaswa kuombea kistokee kwa
gharama yoyote ile.Mwanafalsafa mahiri wa 'Sanaa ya Vita' (Art of War),
Mchina SUN TZU anatahadharisha kuwa "vita ni suala la uhai na kifo,
barabara inayoelekea kwenye usalama au maangamizi..."
Kuna
wanaojidanganya kuwa Rwanda "ni kijinchi kidogo kisicho na uwezo wa
kupambana na Tanzania." I wish wangekuwa sahihi.Kwa mujibu wa SUN TZU,
ushindi katika vita yoyote ile unategemea sana matumizi ya mashushushu
(wapelelezi) wa ndani na wa nje.
Hivi tunafahamu kuwa tuna Wanyarwanda
wangapi Tanzania ambao wapo mahsusi katika kufanikisha azma yoyote ile
ya nchi yao?Kwa maafisa wetu uhamiaji ambao bia mbili tatu tu wapo
tayari kumpa mtu passport ya Kitanzania, tuna maadui wangapi
wanaotengeneza idadi yetu kukaribia milioni 50?
Soma hapa http://suntzusaid.com/book/13 kufahamu
zaidi kuhusu matumizi ya mashushushu katika vita, kwa mujibu wa SUN
TZU.(na jaribu kupigia mstari uhusiano wetu wa Malawi na uwezekano wao
kuwa mojawapo ya aina hizo za mashushushu)
Anyway,
kama nilivyobainisha hapo awali, mie sio nabii wa majanga.Ningependa
sana askari wetu waliokwenda huko DRC watimize jukumu lao haraka na
kurejea nyumbani wakiwa salama WOTE. Nilichoeleza kuhusu PROXY WAR ni
uchambuzi tu unaozingatia hali halisi.
No comments:
Post a Comment