MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, leo imeiaharisha kesi inayomkabili
msanii wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' a.k.a
Annaconda dhidi ya uongozi wa Clouds Media Group hadi Agosti 2, mwaka
huu.
Kesi hiyo ya madai iliyopo mbele ya Hakimu Athumani
Nyamlani, leo ililetwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini ilishindikana
kutokana na wakili anayemtetea, Jaydee kutotokea mahakamani hapo na
kumtuma mwakilishi wake.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa wakili
huyo wa Jaydee, amekwenda katika Mahakama Kuu kuhudhuria kesi nyingine
na hivyo kushindwa kufika mahakamani hapo kuendelea na kesi hiyo na
hivyo kuahirishwa hadi Agosti 2, mwaka huu.
Kesi hiyo ya madai
ilipelekwa mahakamani hapo na Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa
Kampuni ya Clouds Media kwa madai ya kuukashifu uongozi huo.
Kwa
mujibu wa mdai huyo, ambaye ni uongozi wa Clouds Media ulidai kuwa
mdaiwa huyo ambaye ni Lady Jaydee aliandika maneno ya kuukashifu uongozi
huo kupitia blogu yake.
No comments:
Post a Comment