Siku za hivi karibuni mwigizaji anayefanya vizuri kwasasa katika filamu
nchini Niva Zubery amekuwa akiweka status zikimhusu mwigizaji mwenzake
Wema Sepetu na baadhi ya mashabiki wa mastaa hao na wasomaji wa
Swahiliworldplanet kutaka kuupata ukweli kama mastaa hao ni wapenzi kwa
siri au lah.
"nyie swp hembu muulizeni Niva kama mtu wake kwasasa ni
Wema coz status zake ni za kuchombeza kwa bibieee then kama wako close
sana siku hizi, maskini kaka wa watu kaoza kwa wema tayariii !" alisema
shabiki mmoja wa kike aliyekataa kutajwa jina lake.
Status za Niva
zinaonekana kama kuchombeza kitu flani kwa Wema kwa mujibu wa wasomaji
walioitonya SWP.
Baadhi ya status hizo za Niva katika facebook yake ni
hizi hapa "Baaabaa eti wewe upo na wemaa?
(Apana mwanangu) huku akiwa ameweka picha yake mwenyewe na ya mtoto
anayedaiwa kuwa wake", nyingine iko hivi "Niva hanipokerei cm jamaani mwambieni basi kama nampigiaa mwambieeni nawaomba tafazalii" huku akiwa amepost picha ya Wema Sepetu akiwa ameweka simu sikioni".
Status nyingine akiwa ameweka picha hiyo hapo chini wakiwa pamoja na Wema ilisomeka hivi "Etiiiiiii kama tunamuaa kuwa nanihiii na nanihiii itakuwa poa? basi nipe maoni yako ili nijue simmeshajua nilicho maanisha so nataka jibu ili nijue".
Status nyingine akiwa ameweka picha hiyo hapo chini wakiwa pamoja na Wema ilisomeka hivi "Etiiiiiii kama tunamuaa kuwa nanihiii na nanihiii itakuwa poa? basi nipe maoni yako ili nijue simmeshajua nilicho maanisha so nataka jibu ili nijue".
Baadhi ya wachangiaji
walimwambia Niva kuwa wakiwa wapenzi yeye na Wema watapendeza huku
wengine wakimwambia kuwa Wema sio hadhi yake, wengine walimwambia
ajaribu bahati yake kama tayari ameshamzimikia mrembo huyo.
Ili kuupata
ukweli kutoka kwa Niva mwenyewe kama baadhi ya wasomaji walivyotutumia
ujumbe mwanzoni ilibidi kumtafuta Niva jana na kumueleza kila kitu na
yeye alikataa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wema na alipoulizwa kama
kweli sio wapenzi status zake zikionekana kwa mtu wa Wema si zinaweza
kuzua tafrani? Niva alijibu kwa ufupi kwa kusema "hakuna kitu kama hicho
kaka"
No comments:
Post a Comment