Katika Operesheni ya Kuzuia Uhalifu na Madawa ya Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha liliingia kijijini hapo majira ya saa 2 za asubuhi Agosti 13 mwaka huu.
Ilikuwa ni ziara ya kushtukiza
katika kijiji hicho hali iliyowafanya wanakijiji kutaharuki na kuanza kukimbia
na kutokomea milima wakiziacha nyumba zao zikiwa wazi.
Uongozi wa Kijiji hicho nao
ulitoweka kusikojulikana kwa kuhofia mkono wa Jeshi la Polisi.
Kamishna wa Operesheni hiyo ACP
Ngonyani alisema safari hii waliamua kwenda baada ya mavuno kutokana na ukweli
kwamba zikiwa bado shamabni ni kazi nzito sana ya kufyeka.
ACP Ngonyani aliongeza kusema
magunia 225 ya zao hilo haramu nchini Tanzania waliamua kuyateketeza kutokana
na namna ya kuyasafirisha kuwa mgumu.
Mkuu wa Operesheni hiyo alisema
operesheni hiyo bado ni endelevu katika kijiji hicho kwa mwaka huu ni mara ya
pili lakini wamegundua mbinu mpya.
Pia alisema magunia 127 na
watuhumiwa watano wamewasafirisha hadi makao makuu kwa hatua zaidi za kisheria.
Wanakijiji wameilalamikia
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jeshi la Polisi kuwa zao hil ni
muhimu kwa familia zao kwani wanapoliuza husomeshea watoto wao na mahitaji
mengine ya kifamilia.
katika
operesheni hiyo ilishuhudia nyumba moja ya kijana wa kidato cha Nne ikiwa na magunia mawili ya Bangi na baada ya
uchunguzi zaidi mwanafunzi huyo alidai kuwa alivuna ili auze akalipe ada na mahitaji
mengine ya kifamilia.
Imebainika kwamba guni moja
linapouzwa kutoka shambani hutoa kiasi cha zaidi ya shilingi 100,000/= za
Tanzania.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa
wa Arusha Liberatus Sabas amewataja watuhumiwa waliokamatwa katika operesheni
hiyo ambayo imevunja rekodi ya zilizopita kuwa ni Nemali Saitoti (50), Esuba
Daudi (33), Thomas Lesnoi (63), Lomayan Thomas (27) na Natumi Daudi (29).
ACP Sabas amesema opersheni
hiyo ni endelevu na amewataka wananchi, wakulima na watumiaji kuacha kuendeleza
zao hilo kwani ni kinyume cha sheria huku akiwataka kuendeleza Polisi Jamii na
Ulinzi Shirikishi.
No comments:
Post a Comment