HABARI
ZILIZOUFIKIA MTANDAO HUU HIVI PUNDE ZINASEMA KUWA MTU MMOJA
ANAYEKADILIWA KUWA NA UMRI WA MIAKA (45) AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA
YA KUGONGWA NA BASI LA HUD LILILOKUWA LINATOKEA KILOMBERO KUJA JIJINI
DAR, ENEO LA KIEMBENI MIKESE.
IMEELEZWA
KUWA KATIKA AJALI HIYO WATU WENGINE 15 WAMEJERUHIWA WAKATI BASI HILO
LILIPOKUWA LIKIJARIBU KUMKWEPA MTU HUYO NA KUINGIA PORINI NA KISHA
KUPINDUKA MIGUU JUU.
AIDHA
IMEELEZWA KUWA DEREVA WA BASI HILO LILILOSABABISHA AJALI HIYO KUTOKANA
NA MWENDO KASI, ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA HASSAN MBEGA, AMETOROKA NA
JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA ZOEZI LA KUMTAFUTA ILI KUMFIKISHA MBELE
YA SHERIA.
MAJERUHI WAMEPELEKWA KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA MOROGORO KWA MATIBABU.
No comments:
Post a Comment