KLINIKI ya mchezo wa kikapu ya Hasheem
Thabeet imefutwa kwa mwaka huu na Chama cha Mpira wa Kikapu Tanzania
(TBF),kutokana na mchezaji huyo wa NBA kuitwa na klabu yake huko Marekani
kwenda kwenye ratiba maalum.
Akizungumza Dar es Salaam jana Katibu
Msaidizi wa TBF Michael Maluwe, alisema kliniki hiyo imefutwa kwa mwaka huu kwa
sababu Hasheem Thabeet ameitwa na klabu yake kwenye ratiba yao maalum.
"Tumepata taarifa kutoka kwa
uongozi wa Hasheem Thabeet kuwa anatakiwa kurudi nchini kwao mara moja kwenda
kuendelea na ratiba yao ya kuhudhuria katika ligi kuu,"alisema Maluwe.
Maluwe alisema baada ya kumaliza ratiba
hiyo ataelekea Afrika Kusini kuhudhuria Mafunzo ya Vijana wa Afrika maarufu
kama Basketball Without Border (BWB).
Al i s ema ma f u n z o h a y o
anayokwenda kuhudhuria yapo chini ya NBA Afrika na wachezaji wote watakaocheza
katika ligi kuu ya NBA wanahitajika.
Maluwe aliongeza kuwa kliniki hiyo
ilipangwa kufanyika jijini Arusha, ambapo mikoa zaidi ya mitano ilitakiwa
kushiriki ikiwemo Dar es Salaam,Kilimanjaro,Dodoma na visiwa vya Zanzibar.
Kliniki hiyo ambayo hufanyika kila mwaka, mwaka huu
ilipangwa kufanyika Agosti 16 hadi 18 jijini Arusha na kushirikisha vijana
wasiopungua 200
No comments:
Post a Comment