FAMILIA ya Video Queen wa Bongo, Agnes
Gerald Waya ‘Masogange’ inadaiwa kumwachia Mungu ishu ya binti huyo
kukamatwa na madawa ya kulevya Julai 5, mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa ndugu mmoja wa familia
hiyo aliyeomba jina lake lisitiriwe, wameamua kumwachia Mungu ishu hiyo
kwani ndiye anayejua ukweli. “Unajua baba wa Masogange (mzee Gerald
Waya) ni mlokole, sasa amekabidhi ishu nzima mikononi mwa Mungu kwa hiyo
hayuko tayari kusemasema maneno ambayo hayatakuwa na faida,” alisema
ndugu huyo.
Habari zinazidi kudai kwamba, mzee huyo
aliwahi kuchukizwa na kitendo cha binti yake huyo kujiingiza kwenye
sanaa, hadi kuonekana akinengua kwenye muziki.
Hilo liliwahi kubainishwa na Masogange
mwenyewe miaka ya nyuma alipohojiwa na gazeti ndugu na hili (Ijumaa)
kupitia safu ya Ten Questions (Maswali Kumi) ambapo ilikuwa hivi:
TQ: Inasemekana umetokea kwenye familia
ambayo imeiva kidini, walokole, wao wanachukuliaje suala la wewe kuingia
kwenye mambo ya kuuza sura tena wakati mwingine kwenye mavazi ya
kimitego?
Agnes: Mh! Baba yangu hataki kabisa
kusikia mambo ya muziki na niliwahi kukosana naye lakini nalazimisha kwa
kuwa ni moja ya ajira.
Jitihada za kumpata baba wa Masogange ziligonga mwamba baada ya namba iliyotolewa na ndugu huyo kutokuwa hewani.
Masogange na nduguye, Mellisa Edward
walikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, Afrika
Kusini wakiwa na ‘unga’ kilo 150 aina ya crystal methamphetamine wenye
thamani ya shilingi bilioni 6.8.
No comments:
Post a Comment