Ajali
hiyo imelihusisha bus hilo lenye namba za usajili T 729 bes wakati
lilipokuwa likitokea mjini Babati kuelekea mkoani Arusha na kwa mujibu
wa mashuhuda waliokuwa wakisafiri wamesema lilipofika katika eneo
hilo,dereva wa basi hilo alishindishwa kulimudu wakati alipopewa ishara
na wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi wa barabara ya serikali ya
china(Chico) kusubiri lori lililokuwa likishusha matofali kwa ajili ya
ukarabati wa karavati na hatimaye kuyagonga magari yaliyokuwa yakisubiri
lori hilo.
Nae
mganga mfawidhi katika hospitali ya Halmashauri ya mji wa Babati Bw
Mosses Mollel amesema amepokea majeruhi wanane na mpaka sasa amebaki
majeruhi mmoja huku wengine wakiwa wamepata ruksa baada ya kupatiwa matibabu.
No comments:
Post a Comment