Hatimaye mwanadada Jacqueline Wolper ameamua kuweka wazi kilichotokea
mpaka kuamua kubadili Dini yake ya Uislamu na kurudi kwenye ukristo
tena. Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii mwanadada huyu wa
bongo movies ametoa ujumbe ufuatao kwa mashabiki wake.
“…mambo mashabiki zangu.sikua na njia nyingne yakulikwepa hili
nanaamini kua kwa wale mashabk zangu waislam amtomaind maana akuna mtu
wakumsikiliza chin ya hanga zaidi yawazazi so imenipasa kurudi kanisani
kwakauli yawazazi wangu.naamin kama aujaolewa ata uwe na miaka mingap
bado unatakiwa kua chin ya imaya ya wazazi ata ukifa ujue unazikwaje na
mimi ni binadam sijui saa wala dakika.muhm nikuwajuza nakuwaelewesha
mashabk zangu stak maswal nawapenda wote…”
Hapo awali iliripotiwa kuwa mwanadada huyu ameamua kuwa mkristo tena
baada ya penzi lake lililosababisha abadili dini na kuwa muislamu na
jamaa aitwaye 'Dallas' kuvunjika hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment