RAIA 22 wa Ethiopia wanashikiliwa na Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam kwa tuhuma za kuingia nchini bila kibali.
Akizungumza
na Tanzania Daima ofisini kwake jana, Ofisa Uhamiaji Mkoa, Grace
Hokororo, alisema Wahabeshi hao walikamatwa juzi usiku katika maeneo ya
Kinondoni wakiwa katika pagale ambamo walikuwa wamejificha.(HD)
Alisema baada ya wananchi kuwaona waliwatilia mashaka na ndipo walipotoa taarifa polisi ambao walifika na kuwakamata.
"Hii hali
ilikuwa imepoa lakini hivi sasa naona tena wameibuka kwa kweli kazi ipo
na hawa tunategemea kuwasafirisha na kuwarudisha kwao wakiwemo
Wanyarwanda tisa,'' alisema Hokororo.
Alisema
wiki tatu zilizopota jumla ya wahamiaji 42 wakiwemo Wahabeshi, Wasomali
na Wanyarwanda walisafirishwa na kurudishwa makwao.
Alisema
pamoja na jitihada za idara hiyo kuwakamata raia hao, inakabiliwa na
changamoto ya upungufu wa watumishi na magari, jambo alilosema limekuwa
likikwamisha jitihada za idara hiyo katika kutekeleza majukumu yake.
"Watumishi
wengi wamechukuliwa na NIDA na hapa nimebakiwa na wachache na magari
pia ni tatizo tunaiomba serikali iliangalie na ione umuhimu wa
kutuongezea watumishi ili tuweze kufanya kazi vizuri," alisema.
No comments:
Post a Comment