Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Wednesday, November 20, 2013

NDOA YA PACHA WA P-SQUARE YAINGIA DOSARI

Jumapili ya November 17, 2013, jiji la Lagos, Nigeria lilishuhudia harusi kubwa ya kitamaduni kati ya muimbaji wa kundi la P-Square, Peter Okoye na mchumba wake Lola Omotayo, lakini cha ajabu, kaka yake mkubwa, Jude Okoye hakuwepo.
 
Msemaji wa kundi hilo Bayo Adetu alisema Jude hakuwepo kwenye harusi kwakuwa alikwama nchini Ghana.
Jude_okoye-2 Jude Okoye
P-Square walikuwa wametumbuiza jijini Accra, Ghana kwenye show ya ‘Glo and Bounce Slide‘ siku moja kabla ya harusi na hivyo Adetu akadai kuwa Jude alikosa ndege na hivyo kushindwa kurejea Lagos kushuhudia harusi hiyo iliyohudhuriwa na mastaa kibao akiwemo Diamond Platnumz.
 
Lakini chanzo cha sehemu ya kundi la wasanii wengine walioenda Ghana kwenye show hiyo kilisema Jude hakwenda Ghana. 
 
‘Hatukumuona, mapacha hao walikuwa hapa na bendi yao lakini hatukumuona Jude‘, chanzo hicho kilisema.
 
Vyanzo vya ndani kwenye familia ya Okoye vimedai kuwa Jude Okoye na wanafamilia wengine hawakuiunga mkono ndoa ya Peter na mama wa mwanae Lola Omotayo. Vyanzo vingine vimedai kuwa marehemu mama yao naye hakuwa akiuunga mkono uhusiano huo.
dc6c29ec506111e387720e8e429886c3_8 Lola
‘Jude na wengine hawampendi. Hawakutoa baraka zao kwa ndoa hiyo. Hata Paul pia, lakini ni pacha wake. Hata ndugu wengine walikuwepo pale walikuwa wagumu pia kuhudhuria. Jude hakwenda kwasababu hakuwa ameliunga mkono wazo hilo tangu siku ya kwanza,’ chanzo cha familia hiyo kilisema.
LolaOmotayoMakeupLook2_that1960chickdotcom  Lola ni mrembo haswaa
Baadhi ya wanafamilia wa Okoye walienda mbali zaidi na kudai kuwa Lola Omotayo anadaiwa kumsaliti Peter Okoye mara kwa mara. Inadaiwa kuwa walikuwa wanadai vifanyike vipimo vya DNA kubaini kama kweli Cameron na Aliona ni wa Peter kweli ama kashikishwa tu.

Peterrrr 
Peter akiwa na mwanae Cameron
‘Ni serious kabisa, wanadai kuwa Lola hulala na wale anaowaita ‘wajomba’ na wanataka vifanyike vipimo vya DNA, wanataka kumlinda kaka yao.’
   
 
Hata hivyo madai hayo hayajathibitishwa bado.

No comments: