
Miongoni mwa sababu zinazoongeza uzito wa tetesi hizo ni baada ya Tiwa Savage kumpiga chini mmewe kama meneja wake, na kuajiri meneja mpya aitwaye Emeka aka Meka Millions. Tee Billz ndiye aliyekuwa akisimamia kazi za Tiwa.
Chanzo kimoja kimeuambia mtandao wa Sahara Reporters kuwa ndoa ya Tiwa na Tee huenda ikavunjika sababu Tiwa hafurahii tena mapenzi ya mmewe.
Inadaiwa kuwa Tiwa aliwahi kuwa mpenzi wa muimbaji 2Face Idibia, kabla hawajaachana na 2Face kumuoa msichana mwingine aitwaye Annie Macaulay ambaye ndiye mkewe. Pia inasemekana Annie Macaulay (mke wa 2Face) aliwahi kuwa mpenzi wa Tee Billz kabla hawajaachaana na Tee kumuoa Tiwa.
No comments:
Post a Comment