Mkuu
wa Wilaya ya Misungwi Bi. Mariam Lugaila (C) akimkabidhi baiskeli
Mganga mfawidhi wa Kituo cha Afya Mwagiligi kilichopo wilayani humo huku
akishuhudiwa na Meneja Biashara wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Airtel bw.
Ally Maswanya (R).
Msaada huu wa Baiskeli utawasaidia waganga wakuu wa vituo vya tiba wa vijiji 10 kukabiliana na tatizo la usafiri.
Ally Maswanya
Airtel
Tanzania sambamba na kutoa msaada huu wa baiskeli kwa wauguzi pia
imeziwezesha shule mbalimbali nchini kwa misaada ya vitabu, madawati na
vitendea kazi kadha wa kadha kwa lengo la kurejesha shukurani kwa
wananchi na kuisaidia serikali katika harakati zake za maendeleo.
Sehemu ya wauguzi wa Hospitali Kuu Wilaya ya Misungi waliohudhuria makabidhiano hayo.
Mkuu
wa Wilaya ya Misungwi Bi. Mariam Lugaila (C) akimkabidhi baiskeli
Mganga mfawidhi wa Kituo cha Afya Kijima, Dr. Marwa Mwita huku
akishuhudiwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Taknolojia,
Mbunge wa wilaya ya Misungwi Mh. Charles Kitwanga almaarufu 'Mawe
Matatu'.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Bi. Mariam Lugaila akimkabidhi baiskeli Mganga mfawidhi wa Kituo cha Afya Igongwa.
Mkuu
wa Wilaya ya Misungwi Bi. Mariam Lugaila (C) akimkabidhi baiskeli Mussa
Shipemba ambaye alimwakilisha mganga mfawidhi Kituo cha Afya Nyamainza.
Msaada wa baiskeli kutoka Airtel kwa kituo cha Buhunda ukikabidhiwa.
Kaimu Mganga mfawidhi wa Idara ya Afya wilaya ya Misungwi Dr. Beichumila Saula akisoma lisala.
"Tunachangamoto
mbalimbali zinazotukabili ikiwa ni pamoja na uhaba wa fedha kuendeshea
shughuli mbalimbali, Uchache wa watumishi wa kada mbalimbali, Uhaba wa
madawa na vifaa tiba, katika bohari ya dawa ya kanda (MSD), Uhaba wa
usafiri katika vituo vya tiba, Asante Airtel".
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Bi. Mariam Lugaila
"Kwa
niaba ya watu wangu wa Misungwi - Tunawashukuru sana Airtel tukiwasihi
ushirikiano usiishie hapa, uendelee kwani bado kuna mahitaji mengi na
makampuni mengine yaige mfano huu"
Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Tekinolojia ambaye ni Mbunge wa Misungwi Mh.Charles kitwanga nae akitoa shukurani.
No comments:
Post a Comment