Waziri
wa Nishati na Madini Mhe. William Ngeleja (Mb) akizungumza na ujumbe
kutoka Sweden uliomtembelea kwenye ofisi za Wizara ya Nishati na Madini
mapema mchana leo. Ujumbe huo uliongozwa na Waziri wa Biashara wa Sweden
Dkt. Ewa Bjȍrling na Balozi wa Sweden –
Tanzania, Bw. Lennarth Hjelmaker. Nia ya ujumbe huo ni kuangalia fursa
za uwekezaji nchini hususan katika nishati jadidifu (renewable energy), mawasiliano ya simu na mitambo.
Balozi wa Sweden Nchini Bw. Lennarth Hjelmaker akisisitiza jambo mara ujumbe wa Sweden ulipofanya kikao na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. William Ngeleja (Mb.) kwenye ofisi za Wizara mapema leo mchana.
Waziri wa Biashara Sweden Dkt. Ewa
Bjȍrling akimkabidhi Waziri wa Nishati na Madini zawadi mara baada ya
kumalizika kwa kikao kilichoshirikisha ujumbe kutoka Sweden na wataalamu
kutoka Wizara ya Nishati na Madini. Nia ya ziara ya ujumbe huo ni
kubaini fursa za uwekezaji nchini hususan katika nishati jadidifu (renewable energy), mawasiliano ya simu na mitambo.
No comments:
Post a Comment