Mahakama
ya hakimu mkazi Kisutu, leo imeshindwa kumsomea maelezo ya awali,
yaani PH, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania
(ATCL), David Mattaka na wenzake wawili kutokana na mawakili wa upande
wa utetezi kushindwa kufika mahakamani hapo.
Mataka
anakabiliwa na makosa matatu likiwemo kosa la matumizi mabaya ya
madaraka kinyume na Sheria na kifungu 31 Na.11 ya Kuzuia na Kupamba na
Rushwa Na.11 ya mwaka 2007.
Washtakiwa
wengine katika kesi hiyo ni Kaimu Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha
Elisaph Mathew Ikomba na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Ndani, William
Haji.
Katika
shtaka la kwanza linalowahusu washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa
kuwa walishindwa kutunza kumbukumbu za mawasiliano ya manunuzi
waliyokuwa wakifanya na mtoa huduma kinyume na kifungu cha 55 (3), 87
(1) (f) cha Sheria ya Manunuzi ya Umma Na. 21 ya mwaka 2004 na kanuni
ya 17(1) ya Sheria ya Manunuzi (Goods, Works, Non-Consultant Services
and Disposal of Public Asets by Tender) Regulation, G.N. No.97 of 2005.
Upande
wa mashtaka unadai shtaka la pili ambalo pia linawakabili washtakiwa
wote ni la kushindwa kutimiza matakwa ya vifungu vya Sheria ya Manunuzi
ya Umma na Kanuni zake kinyume na kifungu cha 87 (1) (f) cha Sheria ya
Manunuzi ya umma ya mwaka 2004.
Shtaka
la tatu linalo mkabili Mattaka pekee linahusu matumuzi mabaya ya
madaraka kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupamba na
Rushwa ya mwaka 2007
Mara
tu baada ya kesi hiyo kuanza, mapema leo asubuhi upande wa mashtaka
ukiongozwa na mwendesha mashtaka kutoka TAKUKURU, BENY LINCOLYNE,
ulieleza kuwa uko tayari kwa ajili ya kesi hiyo ambapo hata hivyo
hakimu , RITTA TARIMO alilazimika kuiahirisha mpaka Februari 23 mwaka
huu baada ya kuona kwamba mawakili wa utetezi hawakuwemo katika chumba
cha mahakama ilikokuwa ikiendeshwa kesi hiyo.
No comments:
Post a Comment