Wananchi wa Manispaa ya Sumbawanga walihamasika na kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa wa Rukwa katika kampeni hiyo.
Huku
Mkuu wa Mkoa huo akiendelea na ufagiaji wa barabara za Mji huo wa
Sumbawanga Daladala nazo zilikuwa zikiendelea na shughuli zake za
kusafirisha abiria kupitia barabara hizo. Nyuma yake ni Mkuu wa Wilaya
ya Sumbawanga Kanali John Antonyo Mzurikwao.
Waandishi
wa habari nao walikuwepo kutaka kujua kilichomsukuma Mkuu wa Mkoa huo
kuamua kuingia barabarani na kuanza kufagia, ambapo alisema Kiongozi
bora ni lazma afanye kazi kwa vitendo na kuwa mfano bora kwa wale
anaowaongoza.


No comments:
Post a Comment