Kutoka eneo
la tukio mmoja Kati ya abiria walionusurika katika ajali hiyo John
Sanga alisema kuwa dereva wa basi hilo alikuwa akiendesha basi kwa
mwendo kasi na uzembe mwingina hata abiria walipojaribu kumkanya
alishindwa kusikiliza. Katika
ajali hiyo abiria wengine zaidi ya 16 walijeruhiwa vibaya na kulazwa
katika hospital ya wilaya ya Mufindi huku wengine zaidi ya 20 wakipata
michubukomidogo midogo na kutibiwa na kuruhusiwa .Mashuhuda wa ajali
hiyo walimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa ajali hiyo ilitokea
majira ya saa 9 alasiri Leo wakati basi hilo likielekea mkoani Mbeya na
kuwa chanzo ni mwendo kasi na uzembe wa dereva. Alisema
eneo hilo ambalo ajali imetokea ni eneo ambalo linamteremko na kuwa
mbali ya basi hilo kupinduka pia magari mengine Mawili likiwemo gari la
serikali lenye namba za usajili STK 2340 na IT yamegongana na Lori
katika eneo hilo. Maiti zilizotolewa katika ajali hiyo hadi saa 2.usiku
zilikuwa ni nne na hadi mwandishi wa habari hii anatoka eneo la tukio
jitihada za kunyanyua basi hilo ilikutazama maiti nyingine lilikuwa
likieendelea chini ya usimamazi wa mkuu wawilaya ya Mufindi Evarista
Kalalu na mkuu askari wa Kikosi cha usalama barabarani wakiongozwa na
mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa Kedmundi Mnubi
lilikuwa likiendelea . Majeruhi
wa ajali hiyo ambao wamelazwa katika hospital hiyo ya wilaya ya Mufindi
ni pamoja na mtoto wa kiume wa mwaka mmoja ambaye mama yake alikufa
katika ajali hiyo , Alen Kilima mkazi wa Kyela , Mwanahabari wa radio
Kyela Fm Prakseda Mburu (24) ,Maria Mtawa (46) mkazi wa Tukuyu,Lutusyo
Kabenjela (45) mkazi wa Kyela, Elizabeth Andwer(27)Dina Mwasongela (14)
mwanafunzi wakidato cha tatu sekondari ya Lutengano Mbeya,Alex Mwaibambe
(28) mwanafunziwa mwaka wa pili injinia katika chuo kikuu cha Dar es
Salaaam ,Amon Luvanga(30) mkazi wa Mbeya,Yohana Mwasomola(28) Wengine
ni Aggrey Mwangulu (56) mfanyakazi wa TRA Kibaha , Runna Mwampate (36)
mkazi wa Kilawani Dar es Salaam , Iman Mwakifwage (32) mkazi wa Mbeya
Mbali
ya majeruhi hao kulazwa katika Hospital ya wilaya ya Mufindi baadhi ya
majeruhi walikimbizwa katika Hospital ya wilaya ya Ilembula wilayani
Njombe. Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Claus Mwasyeba
alithibitisha kutokeakwa ajali hiyo na kuwa majeruhi Ramadhan Kipangule
(28) mkazi wa TukuyuMbeya amefariki usiku wa leo wakati akipatiwa
matibabu katika Hospital ya wilaya ya Mufindi. Alisema kuwa kati ya
abiria waliokufa katika ajali hiyo watatu ni wanawake na abiria wawili
ni wanaume na mmoja ametambuliwa kwa jina la ramadhan Kipangule (28)
mkazi wa Uyole Mbeya . Hata hivyo alisema kuwa jeshi la polisi
linaendelea kumsaka dereva wa basi hilo Yahaya Abdalla (35) mkazi wa Dar
es Salaam na msaidizi wake Nasib Salum ambao baada ya ajali hiyo
walikimbia.Mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarista kalalu amewataka wananchi
popote pale nchini kujitokeza kutambua miili ya marehemu hao akiwemo
mwanamke huyo aliyeacha mtoto wa mwaka mmoja na nusu.
No comments:
Post a Comment