Mkurugenzi
wa Shughuli za Kanda za Mashariki wa Bohari ya Dawa (MSD), Lucy Nderimo
(kushoto) akimkabidhi Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Angetile Osiah hundi yenye thamani ya sh. mil. 10 ikiwa
ni msaada kwa timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake ya Twiga Stars, katika
hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia makabidhiano hayo
ni Meneja wa Huduma kwa Wateja na Uhusiano wa MSD, Salome Mallamia. Timu
hiyo inapambana na Namibia kesho katika mechi ya marudiano ya kufuzu
fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake. Katibu
Mkuu TFF, Angetile Osiah (kushoto) akitoa shukurani kwa MSD kuipatia
timu hiyo msaada. Kutoka kulia ni Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa
gazeti la Jambo Leo, Grace Michael na Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda za
Mashariki wa Bohari ya Dawa (MSD), Lucy Nderimo Katibu
Mkuu TFF, Angetile Osiah (kushoto) akitoa shukurani kwa MSD kuipatia
timu hiyo msaada. Kulia ni Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda za Mashariki
wa Bohari ya Dawa (MSD), Lucy Nderimo
Mkurugenzi
wa Shughuli za Kanda za Mashariki wa Bohari ya Dawa (MSD), Lucy Nderimo
(kushoto) na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Angetile Osiah wakiwa na furaha wakati wa hafla ya MSD, kukabidhi
msaada wa Sh. Mil. 10 kwa timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake ya Twiga
Stars, Dar es Salaam jana. Katikati ni Meneja wa Huduma kwa Wateja na
Uhusiano wa MSD, Salome Mallamia. Meneja
wa Huduma kwa Wateja na Uhusiano wa MSD, Salome Mallamia (kushoto),
akielezea umuhimu wa msaada huo kwa timu hiyo ya soka kwa wanawake.
Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Angetile Osiah
No comments:
Post a Comment