UHUSIANO wa kimapenzi, ulioanzishwa kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, umesababisha kifo cha mrembo nchini Nigeria.
Habari za mtandaoni zinadai kuwa
mrembo huyo (jina halikutajwa) pamoja na boyfriend wake (jina pia
halijatajwa), walikuwa kwenye uhusiano wa muda mrefu.
Imedaiwa kuwa wakati wawili hao
wakiwa kwenye utekelezaji wa hatua za mwanzo za kufunga ndoa, mrembo
huyo alimtaarifu boyfriend wake kuwa amepata mpenzi mwingine kwa njia ya
Facebook.
Chanzo cha habari kiliiambia
tovuti moja ya nchi hiyo kwamba mrembo huyo alianzisha urafiki wa
Facebook na kijana mmoja raia wa Marekani (jina halijatajwa) kabla ya
kibao kubadilika na kuwa wapenzi.
Chanzo kiliendelea kupasha
habari kwamba mrembo huyo na mpenzi wake wa Facebook, walidumisha
uhusiano wao kwa njia ya mawasiliano ya simu kwa muda mrefu kabla ya
kukata shauri la kuonana ana kwa ana.
“Yule kijana raia wa Marekani
alitembelea Nigeria, akafikia hoteli moja kubwa. Yule mrembo akaenda
kukutana naye na kutumia muda mrefu chumbani.
“Ni kama baada ya kukutana ndiyo
mapenzi yaliongezeka zaidi, kwani alipoondoka hotelini, yule mrembo
alirudi kwa boyfriend wake aliyepanga kufunga naye ndoa na kumueleza
kwamba mapenzi yamekwisha.
“Baada ya kuambiwa hivyo, kijana aliyekuwa na mategemeo ya kufunga ndoa na mrembo huyo, alimpeleleza mpenzi wake na kubaini mahali ambako kijana kutoka Marekani alifikia.
“Baada ya kuambiwa hivyo, kijana aliyekuwa na mategemeo ya kufunga ndoa na mrembo huyo, alimpeleleza mpenzi wake na kubaini mahali ambako kijana kutoka Marekani alifikia.
“Siku iliyofuata alivamia kwenye
ile hoteli, akamkuta mpenzi wake na yule kijana wa Facebook, hapo
ugomvi mkubwa ulizuka. Ugomvi haukuishia hapo kwa sababu kijana wa
Nigeria aliahidi ni lazima aue mtu.
“Siku moja baada ya ugomvi
hotelini, kijana wa Nigeria alimteka mpenzi wake na kumuua kwa
kumkatakata na silaha inayodhaniwa kuwa ni panga,” alisema mtoa habari
huyo.
Kwa mujibu wa mtandao huo mpaka pale habari hiyo inachapishwa, mtuhumiwa wa mauaji alikuwa hajakamatwa.
No comments:
Post a Comment