Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Thursday, January 19, 2012

BECKHAM ASAINI MKATABA MPYA NA LA GALAXY


David Beckham amekiri alikataa ofa nyingi kutoka sehemu mbalimbali duniani na kuamua kusaini mkataba mpya na Los Angeles Galaxy
Mkataba wa miaka mitano wa Beckham na Galaxy uliisha mwezi uliopita na alikuwa anauhusishwa kwa kiasi kikubwa kujiunga na Paris Saint Germain.
Ingawa, ameamua kusaini mkataba mpya wa miaka miwili na LA galaxy, timu ambayo alishinda nayo taji la MLS in 2011.
“Huu ulikuwa uamuzi muhimu zaidi kwangu. Nilikuwa na ofa nyingi sana kutoka sehemu tofauti duniani, lakini kutokana na sababu tofauti ikiwemo mapenzi yangu ya kuendelea kucheza America na kushinda makombe na Galaxy.
“Nimeshuhudia sasa ni jinsi gani soka lilivyo maarufu hapa States na nimeamua kuendelea kushirikiana na wadau wengine kuuukuza huu mchezo hapa.
“Familia yangu na mimi mwenyewe tuna furaha sana hapa, na sasa tunaangalia mbele kuendelea kuishi hapa kwa amani na furaha zaidi.” Alimaliza Beckham.

No comments: